ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Saturday, August 13, 2022
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

Benki ya NMB yazindua kifurushi cha mikopo kwa walimu kanda ya ziwa

I am Krantz by I am Krantz
Jul 12, 2022
in BIASHARA, HABARI, MICHEZO
0
Benki ya NMB yazindua kifurushi cha mikopo kwa walimu kanda ya ziwa
0
SHARES
38
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

RelatedPosts

NMB yaahidi kuendeleza kunufaisha sekta ya kilimo nchini

NMB yaahidi kuendeleza kunufaisha sekta ya kilimo nchini

Aug 10, 2022

NMB Yaibuka Kinara tena Utoaji Huduma Bora Nanenane 2022

Aug 9, 2022

Ufadhili wa NMB wafikia Sh. trilioni 1.56 sekta ya kilimo

Aug 3, 2022
Load More

Mwandishi Wetu

Mwanza. Benki ya NMB Plc imezindua kifurushi maalum cha mikopo yenye riba nafuu kwa walimu kuwawezesha kumudu gharama ya elimu kwa watoto wao, kujiendeleza kitaaluma, kununua vyombo vya usafiri na kulipia bima.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa kifurushi hicho uliofanyika jijini Mwanza mwishoni mwa wiki, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi alisema kupitia kifurushi cha “Mwalimu Spesho” walimu nchini wataondokana na na adha ya mikopo ya mitaani yenye riba kubwa.

“Kupitia kifurushi cha Mwalimu Spesho, walimu watakopa kulipia gharama za elimu kwa watoto au kujiendeleza wenyewe kitaaluma kwa riba nafuu ya asilimia 10,” alisema Mponzi.

Kupitia kifurushi hicho, walimu pia watakopa kwa ajili ya shughuli za kilimo kwa riba ya asilimia tisa pamoja na kukopa kwa ajili ya kununua vyombo vya usafiri ikiwemo pikipiki na kulipia bima.

kabla ya kupokea mikopo, Mponzi alisema walimu hao watapewa bure elimu ya fedha kuwaepusha na matumizi yasiyo ya lazima ili kuhakikisha mikopo hiyo inatumiwa kwa malengo yaliyokusudiwa.

Akizundua kifurushi cha ‘Mwalimu Spesho” katika hafla iliyohudhuriwa na walimu zaidi ya 300 kutoka jijini Mwanza, Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Eng. Robert Gabriel aliipongeza benki ya NMB kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa walimu akisema itawakomboa kutoka kwenye mikopo ya riba kubwa inayotolewa na watu binafsi mitaani.

“Nawasihi walimu watumie vyema fursa ya mikopo kuanzisha miradi ya ujasirimali kujiongezea kipato bila kuathiri utendaji wala kuingilia muda wa kazi,” alisema Gabriel huku akizihimiza taasisi za fedha kuhakikisha zinatoa huduma jumuishi kwa wananchi wa kada zote hadi vijijini.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Wilaya ya Nyamagana, Sholi Maduhu na Mwalimu Grace Muyanja kutoka shule ya msingi Iseni walisema mikopo ya elimu, bima, kilimo na vyombo vya usafiri utaongeza ari ya kazi, ufanisi na utendaji wa walimu na hatimaye ubora kitaaluma na ufaulu wa wanafunzi.

Mwisho….

ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

Related

Tags: NMB
ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

Mkazi wa Mufindi -Iringa akabidhiwa gari mpya Suzuki S Presso baada ya kuibuka mshindi promosheni ya Vodacom Tusua Mapene
BIASHARA

Mkazi wa Mufindi -Iringa akabidhiwa gari mpya Suzuki S Presso baada ya kuibuka mshindi promosheni ya Vodacom Tusua Mapene

by I am Krantz
Aug 13, 2022
Rais Samia Akiwa katika Ziara yake Mkoani Iringa 2022
HABARI

Rais Samia Akiwa katika Ziara yake Mkoani Iringa 2022

by ALFRED MTEWELE
Aug 12, 2022
BIL.11 kupelekwa Mafinga kuboresha miundombinu ya Mji
HABARI

BIL.11 kupelekwa Mafinga kuboresha miundombinu ya Mji

by ALFRED MTEWELE
Aug 12, 2022
Dkt. Mpango Aitaka NEMC na STAMICO Kufanya Tathimini Migodini
HABARI

Dkt. Mpango Aitaka NEMC na STAMICO Kufanya Tathimini Migodini

by ALFRED MTEWELE
Aug 12, 2022
Yanga yaagana na Afisa Habari wao, Hassan Bumbuli
MICHEZO

Yanga yaagana na Afisa Habari wao, Hassan Bumbuli

by ALFRED MTEWELE
Aug 12, 2022
STAMICO YAADHIMISHA MIAKA 50 TANGU IANZISHE
BIASHARA

STAMICO YAADHIMISHA MIAKA 50 TANGU IANZISHE

by ALFRED MTEWELE
Aug 12, 2022

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
July 2022
M T W T F S S
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031
« Jun   Aug »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In