ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Monday, August 8, 2022
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

BENKI YA STANBIC WATILIA MKAZO AHADI YAO KUSAIDIA SEKTA YA ELIMU

I am Krantz by I am Krantz
Jul 17, 2022
in HABARI
0
BENKI YA STANBIC WATILIA MKAZO AHADI YAO KUSAIDIA SEKTA YA ELIMU
0
SHARES
40
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT
Mkuu wa kitengo cha Wateja Binafsi wa benki ya Stanbic, Bw. Omari Mtiga (Kushoto),akikabidhi moja ya madawati 50 yaliotolewa na benki hiyo kwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mh Heri James (Katikati) na Mkuu wa Shule ya Sekondari Kimara Bi Elizabeth Bonzo (Kulia) hivi karibuni. Huu ni muendelezo wa kampeni ya benki hiyo ya Stanbic Madawati Inititaive ambayo inakusudia kutoa madawati 1000 kwa shule mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifuatiwa na upandaji miti, ambayo ni sehemu ya kampeni hiyo inayokusudia kurejesha mfumo wa ikolojia kwa kupanda mti kwa kila dawati lililotolewa.

 

 

RelatedPosts

Mainstream Media Limited Waendesha Mafunzo Maalumu kwa Wakufunzi wa Vicoba  .

Mainstream Media Limited Waendesha Mafunzo Maalumu kwa Wakufunzi wa Vicoba  .

Aug 8, 2022

UKRAINE YAISHTUMU RUSSIA KUSHAMBULIA KIWANDA CHA NYUKLIA

Aug 8, 2022

POLISI WATANO WAUAWA NA WASHAMBULIAJI

Aug 8, 2022
Load More

Dar es Salaam, 17th July 2022: Benki ya Stanbic Tanzania imetilia mkazo ahadi yake ya kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha elimu kwa kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi katika shule za serikali.

.

Benki hiyo ilitoa ahadi hiyo wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Kimara ya kukabidhi madawati 50 yenye thamani ya TZS 4,500,000 milioni, ambayo walikabidhi kwa taasisi hiyo ya elimu.

ADVERTISEMENT

 

Msaada huo ni sehemu ya kampeni inayoendelea ya benki hiyo ilitwayo Stanbic Madawati Initiative, inayolenga kupunguza uhaba wa madawati mashuleni kwa kuchangia madawati nchi nzima na kupanda mti mmoja kwa kila dawati linalotolewa ili kuhakikisha uwiano katika mfumo wa ikolojia wa mazingira.

Madawati hayo yalikabidhiwa na Mkuu wa kitengo cha Wateja Binafsi wa benki ya Stanbic, Bw. Omari Mtiga kwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe.Heri James katika hafla iliyofanyika shuleni hapo mwishoni mwa wiki.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mtiga alisema, ”tunatambua juhudi zinazofanywa na serikali katika kuboresha sekta ya elimu, na tumejipanga kuwa mstari wa mbele kuunga mkono juhudi hizo kwani tunaamini kuwa elimu bora ni muhimu katika kujenga jamii yenye watu wenye uelewa mpana, ambao ni chachu ya maendeleo ya sekta mbalimbali za uchumi wa taifa.”

Aliongeza kuwa dhumuni la benki hiyo kuendelea kujitolea kusaidia sekta ya elimu  ni kusukama gurudumu la maendeleo ya nchi kwa kuunga mkono ndoto za jamii ndani ya maeneo inayofanyia kazi.”Kupata nafasi ya kuchangia maendeleo ya elimu nchini Tanzania ni heshima kwetu kwani tunawawezesha wanafunzi kutimiza ndoto zao na kuchochea kufikia dira ya taifa ya kuleta maendeleo kwa kila mtanzania,” alisema Omari Mtiga.

Akizungumza katika hafla hiyo Mhe. James alisema kuwa mchango wa Benki ya Stanbic ni kielelezo kuwa juhudi za serikali kuweka mazingira rafiki kwa taasisi za fedha na taasisi nyingine kufanya biashara zinazaa matunda, hivyo kuziwezesha taasisi hizo kuwekeza katika jamii.

 

 

ADVERTISEMENT

Mhe. James alisema pamoja na juhudi zake zote, serikali haiwezi kuendeleza sekta zote kwa wakati mmoja kwa asilimia 100 kwa sababu fedha za taifa zinagawanywa kwa sekta zote kulingana na mahitaji. Aliwataka wadau kuunga mkono juhudi za serikali ili kukidhi mahitaji ya wananchi

“Serikali yetu imewekeza katika ujenzi wa madarasa, hata hivyo, kuna uhaba wa madawati, hivyo mchango wa Stanbic wa madawati haya leo unaunga mkono juhudi za serikali za kuboresha mazingira ya elimu katika shule hii, kuwezesha watoto kufikia ndoto zao.” Aliongeza.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi wa serikali za mitaa, wanafunzi wa shule hiyo na wafanyakazi kutoka Benki ya Stanbic.

 

 

 

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

Mainstream Media Limited Waendesha Mafunzo Maalumu kwa Wakufunzi wa Vicoba  .
HABARI

Mainstream Media Limited Waendesha Mafunzo Maalumu kwa Wakufunzi wa Vicoba  .

by I am Krantz
Aug 8, 2022
UKRAINE YAISHTUMU RUSSIA KUSHAMBULIA KIWANDA CHA NYUKLIA
HABARI

UKRAINE YAISHTUMU RUSSIA KUSHAMBULIA KIWANDA CHA NYUKLIA

by Shabani Rapwi
Aug 8, 2022
POLISI WATANO WAUAWA NA WASHAMBULIAJI
HABARI

POLISI WATANO WAUAWA NA WASHAMBULIAJI

by Shabani Rapwi
Aug 8, 2022
TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMATATU AGOSTI 08, 2022
HABARI

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMATATU AGOSTI 08, 2022

by Shabani Rapwi
Aug 8, 2022
ACHA KUNYONYA SEHEMU ZA SIRI WAKATI WA KUFANYA MAPENZI
HABARI

ACHA KUNYONYA SEHEMU ZA SIRI WAKATI WA KUFANYA MAPENZI

by Shabani Rapwi
Aug 7, 2022
NMB Mshiko Fasta kuwanufaisha wakulima
HABARI

NMB Mshiko Fasta kuwanufaisha wakulima

by I am Krantz
Aug 7, 2022

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
July 2022
M T W T F S S
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031
« Jun   Aug »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In