Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema hatojiuzulu nafasi hiyo licha ya wimbi kubwa la Mawaziri walioamua kuachia ngazi kwenye nafasi zao.
–
Boris (58) ameapa kuendelea kung’ang’ana licha ya Mawaziri hao kushindwa kuvumilia kashfa zinazomuandama kwa miezi kadhaa ikiwemo sakata lake la uvunjaji wa sheria ya Uviko-19 jambo lililoighadhabisha umma.
–
Wabunge wamemtaka Boris kujiuzulu lakini amepuuzilia mbali wito huo, akiwaambia: “Kusema ukweli, kazi ya waziri mkuu katika mazingira magumu wakati umepewa mamlaka makubwa ni kuendelea na hilo ndilo nitakalofanya.”