Msanii wa Singeli na mpiga matarumbeta maarufu nchini Kiroboto, inadaiwa amefariki Dunia.
–
Taarifa za kufariki dunia zimetaarifiwa na mtu aliyejitambulisha kwa jina moja la Muhsun, ambaye ni shemeji yake.
Akiongea na Muhsun, amesema kabla ya kifo cha Kiroboto alianguka ghafla wakati akifanya show kwenye hoteli ya Giraffe jijini Dar es salaam.
–
Muhsun amesema baada ya kuanguka alishindwa kuendelea na show, na wakati wakimkimbiza hospitali (hakuitaja) alifariki dunia.
–
Taarifa zinasema mwili wa Kiroboto kwasasa umehifadhiwa katika hospitali ya Temeke, wakati taratibu zingine zikisubiri kwa ndugu wa karibu nanmsanii huyo.
–
Credit : Times Radio FM