ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Monday, March 20, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

DK ASHATU KIJAJI AHAMASISHA KUONGEZA KASI UZALISHAJI WA BIDHAA ZA NDANI KWA VIWANDA HAPA NCHINI

I am Krantz by I am Krantz
Jul 14, 2022
in BIASHARA, BURUDANI, HABARI, MAGAZETI TANZANIA
0
DK ASHATU KIJAJI AHAMASISHA KUONGEZA KASI  UZALISHAJI WA BIDHAA ZA NDANI KWA VIWANDA  HAPA NCHINI
0
SHARES
94
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amewaasa wamiliki wa viwanda kuongeza nguvu na kasi ya kuzalisha bidhaa katika mnyororo mzima wa thamani kama mbolea, sukari, mafuta ya kula na ngano ili kukidhi mahitaji ya ndani, kuuza nje ya nchi, kupunguza uagizaji wa bidhaa hizo nje ya nchi na kujitosheleza hata wakati wa changamoto kama COVID 19 na vita vya Urusi na Ukraine.

RelatedPosts

RJ THE DJ VIFO VINAONGEZA MSONGO WA MAWAZO

ROMY JONS AOMBA MSAMAHA

Mar 20, 2023

MCHUNGAJI AFUNGA KANISA KISA ASHINDA MIL 100 ZA “KUBETI”

Mar 20, 2023

WAZIRI BITEKO ATAKA BAJETI YA 2023/24 KUZINGATIA VIPAUMBELE VYA WIZARA

Mar 20, 2023
Load More

Waziri Kijaji ameyasema hayo Julai 14, 2022 katika Mkutano na Wanachama wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) katika ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. Mkutano huo ulilenga kujadiliana mambo ya kipaumbele kwa maendeleo ya Sekta ya Viwanda katika ukuaji wa uchumi wa nchini.

 

Aidha, Waziri Kijaji amewashauri Wanachama wa Shirikisho hilo kizalisha kiushindani bidhaa zenye ubora na viwango vinavyotakiwa ili ziweze kuingia katika soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) na Eneo Huru la Biashara Barani Afrika pamoja (AfCFTA) na Dunia kwa ujumla ili kutimiza lengo la Serikali la kuifanya Tanzania kuwa lango la biashara Afrika.

ADVERTISEMENT

Dkt. Kijaji pia amesema Wizara itaendelea kushirikiana na Wizara ya Kilimo katika kuhakikisha upatikanaji wa malighafi za viwandani pamoja na Sekta Binafsi katika kuendeleza Sekta ya viwanda nchini inayotegemewa kuongeza thamani malighafi, kuongeza ajira, pato la taifa, kuongeza fedha za kigeni na kukuza uchumi wa taifa kwa ujumla.

 

 

 

Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) Bw. Paul Makanza ameishukuru Serikali kwa hatua mbalimbali iliyozichukua kupitia Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara ikiwemo marekebisho ya Sheria, kuanzisha mifumo mbalimbali ya kutoa huduma kielektroniki, kufuta ada na tozo pamoja na ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya barabara, umeme, reli ya kisasa na diplomasia ya kiuchumi.

Pamoja na hayo Bw. Makanza ameiomba Serikali kutekeleza Mpango huo wa Maboresho kwa haraka, kulinda maboresho yaliyofanyika kwa kuzingatia kutokuanzisha ada au kodi mpya itakayokuwa kero pamoja na kulinda bidhaa zinazozalishwa nchini huku ikisimamia ushindani wa biashara wa haki pamoja na kupunguza ushuru wa malighafi za mafuta ya kula ili kuongeza uzalishaji na kuuza mafuta hayo kwa bei rahisi

ADVERTISEMENT

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

RJ THE DJ VIFO VINAONGEZA MSONGO WA MAWAZO
HABARI

ROMY JONS AOMBA MSAMAHA

by Shabani Rapwi
Mar 20, 2023
MCHUNGAJI AFUNGA KANISA KISA ASHINDA MIL 100 ZA “KUBETI”
HABARI

MCHUNGAJI AFUNGA KANISA KISA ASHINDA MIL 100 ZA “KUBETI”

by ALFRED MTEWELE
Mar 20, 2023
WAZIRI BITEKO ATAKA BAJETI YA 2023/24 KUZINGATIA VIPAUMBELE VYA WIZARA
HABARI

WAZIRI BITEKO ATAKA BAJETI YA 2023/24 KUZINGATIA VIPAUMBELE VYA WIZARA

by Shabani Rapwi
Mar 20, 2023
TMA YATOA TAHADHARI MVUA KUBWA MIKOA HII KUANZIA LEO NA KESHO
HABARI

TMA YATOA TAHADHARI MVUA KUBWA MIKOA HII KUANZIA LEO NA KESHO

by Shabani Rapwi
Mar 20, 2023
WATU 5 WASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA WIZI MAFUTA SGR
HABARI

WATU 5 WASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA WIZI MAFUTA SGR

by ALFRED MTEWELE
Mar 20, 2023
MARUFUKU KUTOA FEDHA UPATE DHAMANA POLISI
HABARI

MARUFUKU KUTOA FEDHA UPATE DHAMANA POLISI

by Shabani Rapwi
Mar 20, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
July 2022
M T W T F S S
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031
« Jun   Aug »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In