Waziri wa Afya, Ummy Mwalimuamesema hadi kufikia asubuhi ya leo tarehe 29 Julai 2022, idadi ya Wagonjwa waliothibitishwa kuugua ugonjwa wa Homa ya Mgunda nchini ni 20 na na kati yao watatu wamefariki.
–
“Hivi sasa hakuna mgonjwa aliyelazwa wote wameruhusiwa kurudi nyumbani na wanaendelea na shughuli zao, hii inaendana na sayansi inayojulikana kwa ugonjwa huu kuwa ugonjwa huu unatibika kwa kutumia dawa ambazo zinapatikana katika vituo vya kutolea huduma za afya kote nchini”
–
“Aidha, Timu ya ufuatiliaji imebaini kuwa, miongoni mwa Watu waliotangamana na Wagonjwa hao (contacts) hakuna aliyeonyesha dalili za ugonjwa huu hadi kufikia sasa, hii inadhihirisha pia, ni mara chache ugonjwa huu huambikizwa kutoka Binadamu mmoja kwenda kwa mwingine”