Nchi ya India ndio inaongoza duniani kuwa na watumiani wengi wa Instagram wakifikia milioni 253.5, kisha Marekani milioni 155.7, Brazil milioni 122.5, Indonesia milioni 99.9, Uturuki milioni 54.4 na Japan milioni 47.3.
–
Na kati ya watumiaji wa Instagram duniani kote ambao ni bilioni 1.4, asilimia48.1 ni wanawake, huku wanaume wakiwa asilimia 51.9.
–
Baada ya kuanzishwa Instagram hapo mwaka 2010 ulipata watumiaji milioni 1 ndani ya miezi miwili, hadi kufikisha mwaka mmoja tayari ilikuwa na watumiaji milioni 10, hadi sasa unatumika katika lugha 32 duniani kote.
–
Facebook ndio mtandao wenye watumiaji wengi kwa mwezi ambao ni bilioni 2.9, YouTube bilioni 2.5, WhatsApp bilioni 2, Instagram bilioni 1.4, WeChat bilioni 1.2 na TikTok bilioni 1.