Mahakama ya hakimu Mkazi Mkoa wa Katavi imewakuta na hatia Bwana Beno Mathias Msimbe na mwenzake Nova Isack Mazeba kwa kosa la kukutwa na nyara za serikali ambazo ni meno ya tembo mawili yenye thamani ya tsh 52,948,540.92 mali ya Jamhuri ya muungano wa tanzanzia.
–
Shauri hilo la uhujumu uchumi na 3/2022 limesikilizwa katika mahakama ya hakimu mkazi Katavi mbele ya Hakimu Gway Sumaye. Akisoma hukumu hiyo amesema upande wa mashtaka umethibitisha mashtaka hayo bila kuacha shaka.
–
Hivyo mahakama imewatia hatiani na kuamuru wafungwe jela miaka 20 , pia meno hayo mawili yameamuriwa kurudishwa serikalini.