Msemaji wa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC, Haji Manara, amekubali kuomba msamaha kwa Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Wallace Karia.
–
Manara amedai kwake kuomba radhi ni kitu cha kiungwana na sio ushamba kama wengine wanavyodhani. “Hata kama yeye ndiye alinianza lakini naomba msamaha, kwa namna yoyote ile nilikosea kujibizana na Rais wa mpira naomba radhi”
–
Hata hivyo amesema, yupo tayari kwa lolote kutoka kwenye mamlaka husika, lakini kitu cha msingi kilikuwa ni kuomba radhi kwa kiongozi wa soka la nchi. ”Kama itaonekana nastahili kuchukuliwa hatua nipo tayari kupokea adhabu hiyo. Lakini lazima niombe msamaha bila kujali kamati itaamua nini” Alisema Manara.