Jasin Bushi, kijana mwenye umri wa miaka 18 amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la kudukua akaunti za Snapchat na kulaghai.
–
Jasin alikiri kuingia kwenye komputa bila idhini ya mmiliki wake na kudukua akaunti hizo pia kuzitumia kulaghai na kujipatia pesa.
–
Kati ya Disemba 2020 na Februari 2021 Jasin alidukua akaunti 7 za Snapchat za wanawake na kuzibadili password.
–
Baada ya kufanya hivyo alianza mawasiliano na marafiki wa wanawake hao akijifanya kuwa na shida ya pesa. Uchunguzi ulibaini kuwa Jasin alikuwa na tabia hizo baada ya kumkuta na akaunti nyingi feki zikiwemo za PayPal.