Mtumishi wa shirika la umeme TANESCO anaefahamika kwa jina la Yahaya Abdul Mkazi wa Manispaa ya Mpanda mkoa wa katavi amekutwa amefariki Dunia katika nyumba ya kulala wageni alikoenda kujipumzisha na Mwanamke anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake.
–
Tukio hilo Ambalo limetokea Mtaa wa Ikulu kata ya Kawajense, Diwani wa kata hiyo Uwezo Bachu amesema baada ya kuona Umati wa watu ukiwa umezunguka Nyumba ya kulala wageni ndipo alipofika na kuelezwa kuwa Marehemu aliingia kwenye Nyumba hiyo akiwa na Rafiki yake wa kike.
–
Mhudumu wa Nyumba ya kulala wageni ameeleza kuwa Marehemu alifika majira ya saa saba mchana na Mwanamke huyo lakini alishanganzwa kuona pikipiki ya mtu huyo mpaka asubuhi ikiwa pale gesti
–
Kwa upande wake afisa uhusiano wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa katavi Emanuel Tinda amekiri kupokelewa kwa mwili wa mtu ambaye jina lake halijafahamika na uchunguzi wa Kitabibu ili kubaini kifo chake unaendelea.