ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Monday, August 8, 2022
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

NBC YAJIVUNIA MAFANIKIO SABA MSIMU WA KWANZA WA LIGI KUU YA NBC PREMIER LEAGUE

Shabani Rapwi by Shabani Rapwi
Jul 8, 2022
in HABARI
0
NBC YAJIVUNIA MAFANIKIO SABA MSIMU WA KWANZA WA LIGI KUU YA NBC PREMIER LEAGUE
0
SHARES
45
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

ADVERTISEMENT

 

RelatedPosts

Mainstream Media Limited Waendesha Mafunzo Maalumu kwa Wakufunzi wa Vicoba  .

Mainstream Media Limited Waendesha Mafunzo Maalumu kwa Wakufunzi wa Vicoba  .

Aug 8, 2022

UKRAINE YAISHTUMU RUSSIA KUSHAMBULIA KIWANDA CHA NYUKLIA

Aug 8, 2022

POLISI WATANO WAUAWA NA WASHAMBULIAJI

Aug 8, 2022
Load More
ADVERTISEMENT

 

Benki ya NBC imetaja mafanikio saba makubwa yaliyotokana na uamuzi wake wa kudhamini ligi kuu ya soka Tanzania bara ‘NBC Premier League’ ikiwamo kuimarika kwa mnyororo wa uchumi, ajira pamoja na kuimarika kwa mazingira ya wachezaji na vilabu.
–
Mwezi Okotoba mwaka jana (2021) Benki hiyo ilichukua uamuzi mzito wa kudhamini ligi kuu Tanzania Bara kwa mkataba wa miaka mitatu ambapo wadau walikuwa na maoni mbalimbali juu ya uamuzi huo.
–
Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa wachezaji na vilabu vilivyoshiriki ligi kuu msimu wa 2021/2022, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi alisema uamuzi huo umezaa matunda makubwa kwa benki, tasnia ya michezo pamoja na taifa kwa ujumla.
“Mchango ambao udhamini huu umeleta kwa taifa letu unatupa sisi Benki ya NBC, kama Benki ya kizalendo inayomilikiwa kwa kiasi kikubwa na Serikali yetu, wasaa wa kusimama kifua mbele, na kujivunia kuweza Kufungua fursa za maisha kwa watanzania wenzetu na kusaidia kupambana na umasikini,” alisema Sabi.
–
Alitaja manufaa hayo ikiwa kuimarika kwa biashara na mnyororo wa uchumi ambapo alieleza kuwa timu 16 zilizoshiriki kwenye Ligi Kuu ya NBC zimesaidia kuboresha biashara katika miji yao na hivyo kukuza vipato vya familia kupitia mauzo ya bidhaa na huduma mbalimbali.
–
Kuhusu ajira alisema ligi ya NBC imesaidia kutoa ajira 3,000 za moja kwa moja kwa wachezaji, waamuzi, wauguzi, walimu na wanahabari wa michezo.
–
Aidha, alisema ligi hiyo imesaidia katika kuongeza makusanyo ya kodi kwa Serikali kupitia mauzo ya tiketi, kodi za ongezeko la thamani na kupitia mishahara ya wachezaji na viongozi.
–
“Benki ya NBC pia inajivunia kutumia jukwaa hili katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika ujumuishaji wananchi katika sekta rasmi ya fedha. Kupitia mechi za ligi hii, tumefanikiwa kufungua akaunti mpya, kutoa elimu ya fedha na mikopo ya uwezeshaji kwa maelfu ya wananchi,” alisema Sabi.
–
Eneo jingine ni kuwezesha upatikanaji wa bima kwa wachezaji na viongozi ambapo imesaidia kuongeza hamasa na uhakika wa ajira zao. Pia, alitaja eneo la kuibua vipaji ambapo alisema ligi hiyo imekuwa na mchango mkubwa katika kuibua vipaji akiwataja wachezaji kama Reliants Lusajo wa Namungo FC na Abdul Sopu wa Coastal Union ambao wameng’ara kupitia ligi hiyo.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa alisema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuboresha mazingira ya soka nchini. “Hili ni jambo la kujivunia na ni matumaini yetu kuwa tutapiga hatua kubwa kisoka duniani” alisema.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia alisema ligi kuu ya mwaka huu imekuwa bora zaidi kutokana na maandalizi mazuri na udhamini mzuri huku akiwapongeza washindi.
–
“TFF inawapongeza washindi wote kwenye ligi kuu na kombe la shirikisho na waliopanda kushiriki Ligi kuu nasi tutatoa ushirikiano kwa timu zote zitakazoshiriki,” alisema.

Related

ADVERTISEMENT
Shabani Rapwi

Shabani Rapwi

Shabani Rapwi (Kijana Mchapa Kazi) WhatsApp; 0689232546 Email ;shabanimohamed932@gmail.com

Related Posts

Mainstream Media Limited Waendesha Mafunzo Maalumu kwa Wakufunzi wa Vicoba  .
HABARI

Mainstream Media Limited Waendesha Mafunzo Maalumu kwa Wakufunzi wa Vicoba  .

by I am Krantz
Aug 8, 2022
UKRAINE YAISHTUMU RUSSIA KUSHAMBULIA KIWANDA CHA NYUKLIA
HABARI

UKRAINE YAISHTUMU RUSSIA KUSHAMBULIA KIWANDA CHA NYUKLIA

by Shabani Rapwi
Aug 8, 2022
POLISI WATANO WAUAWA NA WASHAMBULIAJI
HABARI

POLISI WATANO WAUAWA NA WASHAMBULIAJI

by Shabani Rapwi
Aug 8, 2022
TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMATATU AGOSTI 08, 2022
HABARI

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMATATU AGOSTI 08, 2022

by Shabani Rapwi
Aug 8, 2022
ACHA KUNYONYA SEHEMU ZA SIRI WAKATI WA KUFANYA MAPENZI
HABARI

ACHA KUNYONYA SEHEMU ZA SIRI WAKATI WA KUFANYA MAPENZI

by Shabani Rapwi
Aug 7, 2022
NMB Mshiko Fasta kuwanufaisha wakulima
HABARI

NMB Mshiko Fasta kuwanufaisha wakulima

by I am Krantz
Aug 7, 2022

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
July 2022
M T W T F S S
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031
« Jun   Aug »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In