Mshambuliaji wa PSG, Neymar anafikiria kuondoka klabuni hapo msimu huu wa joto, baada ya kugundua kuwa klabu hiyo ina furaha kwa yeye kuondoka.
–
Mawasiliano yamefanywa na Chelsea, mojawapo ya klabu chache iliyoonyesha nia ya kumsajili Neymar, kutokana na nia ya mmiliki mpya Todd Boehly kutoa kauli kubwa katika soko la usajili msimu huu wa joto.
–
Wakati huo huo, mchezaji mwenzake wa Brazil na rafiki wa karibu, Thiago Silva amezungumza na Neymar kujiunga naye Stamford Bridge. Hata hivyo, inabakia kuonekana ikiwa Chelsea na Thomas Tuchel wana nia ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30.
–
Neymar alisaini mkataba mpya na PSG miezi 12 iliyopita, na mshahara wa kila mwaka ni Euro milioni 43 bila bonasi, na amebakiza miaka mitano katika mkataba huo sasa baada ya kuripotiwa kipengele cha kuongeza hadi 2027.