Nyota wa soka kutokea Brazil Neymar atasimama Mahakamani mwezi Oktoba kwa tuhuma za ulaghai na rushwa kuhusiana na uhamisho wake kutoka klabu ya Santos kwenda klabu ya Barcelona mwaka 2013.
–
Kampuni ya Brazil Investment Group DIS iliyokuwa ikimiliki sehemu ya haki za uhamisho za nyota huyo imedai kuwa ilipokea ada ndogo kuliko ilivyostahili huku pesa nyingine ikifichwa.
–
Watuhumiwa wengine katika kesi hiyo ni pamoja na wazazi wa Neymar, meneja wa zamani wa Santos Odilio Rodriguez, pamoja na aliyekuwa Rais na Makamu wa Rais wa Barcelona Sandro Rosell na Josep Maria Bartomeu.