ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT
Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kufuatia ajali ya basi dogo la shule iliyotokea mkoani Mtwara na kusababisha vifo vya watu kumi, nane wakiwa ni wanafunzi wa shule ya msingi ya King David.
–
Katika salamu za pole alizozitoa kupitiwa ukurasa wake wa Twitter, Rais Samia amesema amesikitishwa na vifo hivyo na anawapa pole wafiwa, mkuu wa mkoa pamoja na jamaa, na kwa majeruhi amewaombea kwa Mwenyezi Mungu awaponye.
