Mchezaji mpya wa Tottenham Hotspurs, Richarlison, ataukosa mchezo wa ufunguzi Ligi Kuu England msimu ujao dhidi ya Southampton, baada ya kupata adhabu ya kufungiwa mchezo moja kwa kosa la kutupa moto (fataki), akiwa na Everton msimu uliopita.
–
Mbrazil huyo ambaye alijiunga na Spurs kwa pauni milioni 60 wiki iliyopita, alishtakiwa na Chama cha Soka mwezi uliopita kwa kisa hicho kilichotokea baada ya kufunga bao la ushindi dhidi ya Chelsea kwenye Uwanja wa Goodison Park.
–
Richarlison alisherehekea bao lake la dakika ya 46 kwa kuokota moto (fataki), ambao ulikuwa umetua uwanjani na kuurusha tena kwa mashabiki.
–
FA sasa wamehitimisha uchunguzi wao na kumpa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 adhabu ya kuukosa mchezo mmoja na faini ya pauni 25,000.