Star wa muziki na mitindo, Rihanna ametajwa kuwa ndiye bilionea wa kike mwenye umri mdogo zaidi ambaye amejitengenezea utajiri wake mwenyewe. [Self-Made Billionaire]
–
Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 34 kwa mara nyingine tena amepata nafasi kwenye orodha ya kila mwaka ya jarida la Forbes la wanawake matajiri zaidi waliojitengenezea utajiri wao wenyewe. Hii ni mara yake ya tatu kuingia katika orodha hiyo, ambapo anashika nafasi ya 21.
–
Rihanna ndiye bilionea pekee chini ya umri wa miaka 40 na ana utajiri wa dola bilioni 1.4 (zaidi ya Tsh. Trilioni 3), huku mwonekano wake mzuri, kampuni zake za mitindo “Fenty Beauty”, Fenty Skin, na Savage X Fenty zimehusika kwa kiasi kikubwa, na pia mapato kutokana na kazi za muziki na filamu.
–
CNBC imeripoti kwamba sehemu kubwa ya utajiri wake hutoka kwenye kampuni ya Fenty Beauty, ambayo iliingiza dola milioni 550 katika mapato mnamo 2020. Kampuni hiyo ina ubia wa 50-50 na kampuni kubwa kama LVMH, Moët Hennessy na Louis Vuitton.