Bondia mkongwe Mike Tyson ametoa kauli ya kushtua na kushangaza kwa kudai siku yake ya kufa imekaribia sana.
–
Akiongea kupitia Podcast yake, Mike Tyson amesema: “Sote tutakufa siku moja bila shaka. Kila ninapojitazama kwenye kioo naona madoa madogo usoni mwangu, hiyo ina maana siku yangu ya mwisho wa kuishi inakaribia, iko karibu sana’.”
–
Gwiji huyo wa ndondi mwenye miaka 56 amekuwa akihusishwa mara kwa mara na kurudi tena ulingoni katika miezi ya hivi karibuni kuzichapa na Jake Paul.
–
Tyson amekua mtulivu miaka ya hivi karibuni huku akitafakari juu ya maisha yake ya zamani amesema pesa hazijawahi kumfanya aridhike na maisha.
–
“Pesa haimaanishi chochote kwangu, siku zote mimi huwaambia watu wanafikiria pesa itawafurahisha, hawajawahi kuwa na pesa hapo awali”.