Timu ya Singida Big Stars imethibitisha kukamilisha usajili wa kiungo Aziz Andambwile kutoka Mbeya City.
–
Big Stars imethibitisha hilo kupitia kwenye ukurasa wao wa mtandao wa kijamii wa Instagram, kwa kuweka picha ya mchezaji huyo na ujumbe unaosomeka.
–
“Ni kiungo mwenye uwezo wa kucheza nafasi tofauti tofauti uwanjani. Mchezaji kijana, mzawa, msomi, mpambanaji wa kweli akiwa na timu yake mpaka timu ya Taifa.
–
“Pia ni mtaalamu wa pasi na mashuti ya mbali.Ameshacheza Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na timu ya Big Bullet ya Malawi. Kwa sasa ni Kiungo Mkabaji anayetegemewa na Timu ya Taifa #TaifaStars. Karibu Singida Big Stars FUNDI Aziz Andabwile Mwambalaswa”