Msanii wa hip hop nchini Kenya, Stivo Simple Boy ameshangazwa na watu wanaotumia condom wakiwa faragha.
–
Amesema ni kinyume na maagizo ya kidini kwani hata katika biblia vitu hivyo havijatajwa hivyo haelewi kwanini watu wanaviendekeza kutumia badala ya kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu tu
–
Ikumbukwe, Stivo Simple Boy katika mahojiano yake ya nyuma alisema aliachana na msichana wake Pritty Vishy kwasababu ya ishu za kutaka kufanya mapenzi kabla ya ndoa kwani rapa huyo aliwahi kuweka wazi kuwa yeye bado ni bikira
–
Stivo aliwahi kukiri kuwa mwanamke anayemhusudu zaidi ni Wema Sepetu na angekuwa na uwezo angekuwa mrembo huyo wa Kibongo aliyewahi kuwa Miss Tanzania.