Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 28.07.2022

Cristiano Ronaldo ameiambia Manchester United kwamba anataka kuachiliwa kusitisha kandarasi yake ili kuchezea timu inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya lakini United wamekariri kuwa hawataki kumuuza mshambuliaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 37.
–
Dili la mshambuliaji wa Liverpool Roberto Firmino linaripotiwa kuwa “karibu sana” huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 akitarajiwa kuhamia Juventus katika ligi ya Serie A.
–
Hatua hiyo inaweza kusimamisha harakati za Juventus kumnunua mshambuliaji wa Chelsea na Ujerumani Timo Werner, 26, na mshambuliaji wa Manchester United na Ufaransa Anthony Martial, 26.

Beki wa kushoto wa Uhispania Alex Grimaldo, 26, ndio chaguo kuu kwa Manchester City, huku Benfica ikiweka bei ya euro 20m kwa uhamisho wake.
–
Bournemouth wamekubali mkataba wa pauni milioni 15 kumsaini kiungo wa kati wa Middlesbrough Muingereza Marcus Tavernier, 23. Nottingham Forest inavutiwa na kiungo wa kati wa Real Betis na Ureno William Carvalho, 30.

Barcelona wanakaribia kuipiku Chelsea katika kumsajili Jules Kounde, 23, baada ya kuafikiana na Sevilla kwa ada ya euro 50m kumnunua mlinzi huyo wa Ufaransa.
–
Uhamisho wa mkopo wa Nuno Tavares kutoka Arsenal kwenda Atalanta uko mashakani baada ya timu hiyo ya Italia kukataa ombi la The Gunners la mkopo wa moja kwa moja na mpango wa kumnunua beki huyo wa kushoto wa Ureno mwenye umri wa miaka 22.
–
Manchester United bado wana matumaini ya kumsajili kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong, 25, kutoka Barcelona.

Paris St Germain walimsajili mshambuliaji wa Italia Gianluca Scamacca, 23, kabla ya kukamilisha uhamisho wake wa kwenda West Ham kutoka Sassuolo. Mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez, 35, ametia saini mkataba na Nacional.