
Chelsea wanajiandaa kuwasalimisha mabeki wa pembeni wa Uhispania Cesar Azpilicueta, 32, na Marcos Alonso, 31, pamoja na pauni milioni 51 ili kuwashinda Manchester United katika mbio za kumsajili kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong, 25.

Manchester United wako tayari kusikiliza ofa kwa Cristiano Ronaldo msimu huu wa joto huku Chelsea na Napoli wakimtaka mshambuliaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 37.
–
Tottenham wanakaribia kukamilisha usajili wa beki wa kati wa Barcelona na Ufaransa Clement Lenglet, 27, kwa mkataba wa mkopo wa msimu mzima.

Manchester United wametakiwa kulipa ada ya uhamisho ya pauni milioni 106 ili kuwasajili mlinzi wa Argentina Lisandro Martinez, 24, na winga wa Brazil Antony, 22, kutoka Ajax.
–
Mkufunzi wa Brentford Thomas Frank anasisitiza kuwa klabu ya London Magharibi haikati tamaa katika kumsajili kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 30, ambaye anatarajiwa kujiunga na Manchester United.
–
Arsenal wanafikiria kumnunua beki wa kushoto wa Benfica Mhispania Alex Grimaldo, 26, huku Mikel Arteta akitamani kuongeza ulinzi kwa Kieran Tierney.
Chelsea wanatazamia kumpa beki wa pembeni wa England Reece James, 22, nyongeza ya kandarasi, licha ya mkataba wake wa sasa kukamilika Juni 2025, ili kuzuia nia ya Manchester City na Real Madrid.
–
Chelsea bado wanapewa nafasi kubwa ya kumsajili Raphinha kwa pauni milioni 55, huku Leeds bado wakisubiri ofa kutoka kwa Barcelona kwa ajili ya kumnunua mshambuliaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 25.
–
Mshambulizi wa Ureno Fabio Silva, 19, anatazamiwa kujiunga na Anderlecht kwa mkopo wa msimu mzima kutoka Wolves, ambao walimnunua kwa £35m miaka miwili iliyopita.

Leeds wako tayari kulipa kiasi cha kuvunja rekodi ya klabu cha £31.6m kumsajili mshambuliaji wa Ubelgiji Charles de Ketelaere kutoka Club Bruges, 21.
–
Kiungo wa kati wa Arsenal Muingereza Matt Smith mwenye umri wa miaka 21 anasakwa na vilabu vingi vya Championship vikiwemo Millwall na Luton msimu huu wa joto.
–
Newcastle bado wako kwenye mazungumzo na Everton kuhusu uwezekano wa kumnunua winga Mwingereza Anthony Gordon, 21.
–
Norwich City wanavutiwa na mshambuliaji wa Manchester City na Colombia Marlos Moreno, 25.