Chelsea wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Manchester United, Cristiano Ronaldo, ambaye amewaarifu mashetani wekundu kuwa anataka kuondoka msimu huu wa joto. Ronaldo, 37, anaweza kuwa tayari kujiunga na Chelsea, lakini The Blues bado hawajaamua kutoa ofa rasmi kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno.
–
Rais wa Barcelona Joan Laporta na wakala Jorge Mendes pia wanajadili uwezekano wa nyota wa zamani wa Real Madrid, Ronaldo kurejea La Liga. Ronaldo pia yuko tayari kupunguza mshahara wake wa pauni 500,000 kwa wiki kwa Manchester United.
–
AC Milan wanashughulikia mpango wa kumsajili winga wa Chelsea kutoka Morocco Hakim Ziyech, 29, kwa mkopo.
–
Maafisa wa Manchester United walikutana na wenzao wa Ajax wikendi kujadili kuhusu mkataba wa kumnunua mlinzi wa kimataifa wa Argentina Lisandro Martinez, 24, huku Red Devils wakitoa pauni milioni 39.6.
–
Tottenham wamefanya uchunguzi kumnunua mshambuliaji wa kimataifa wa Uholanzi wa Barcelona Memphis Depay, 28, ambaye anaweza kuondoka Nou Camp kwa pauni milioni 17.
–
Everton na West Ham zote zimesajili nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Albania Armando Broja, 20, kutoka Chelsea, huku mshambuliaji huyo akiwa na thamani ya £30m.
–
Leeds pia wanakaribia kufikia makubaliano ya pauni milioni 20 ikiwa ni pamoja na nyongeza za mchezaji wa kimataifa wa Marekani wa RB Leipzig Tyler Adams, 23, kama mbadala wa Kalvin Phillips baada ya Mwingereza huyo kujiunga na Manchester City.
–
Crystal Palace, Southampton na Nottingham Forest zote zinavutiwa na kiungo wa kati wa zamani wa kimataifa wa Uingereza Morgan Gibbs-White, 22, kutoka Wolves.
–
Chelsea wako kwenye mazungumzo ya juu na Manchester City kwa ajili ya kumnunua mshambuliaji wa England Raheem Sterling, 27, ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa £50m na mabingwa hao wa Premier League.
–
Newcastle bado wana nia ya kumsajili winga wa kimataifa wa Ufaransa Moussa Diaby, 22, kutoka Bayer Leverkusen.
–
West Ham wamekuwa na ofa ya pauni milioni 20 kwa kiungo wa kimataifa wa Ubelgiji Amadou Onana, 20, iliyokataliwa na Lille.