ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Saturday, August 13, 2022
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

UJERUMANI YAIFATA ENGLAND FAINALI

Shabani Rapwi by Shabani Rapwi
Jul 28, 2022
in HABARI
0
UJERUMANI YAIFATA ENGLAND FAINALI
0
SHARES
13
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

 

RelatedPosts

Mkazi wa Mufindi -Iringa akabidhiwa gari mpya Suzuki S Presso baada ya kuibuka mshindi promosheni ya Vodacom Tusua Mapene

Mkazi wa Mufindi -Iringa akabidhiwa gari mpya Suzuki S Presso baada ya kuibuka mshindi promosheni ya Vodacom Tusua Mapene

Aug 13, 2022

Rais Samia Akiwa katika Ziara yake Mkoani Iringa 2022

Aug 12, 2022

BIL.11 kupelekwa Mafinga kuboresha miundombinu ya Mji

Aug 12, 2022
Load More

 

Ujerumani imeichapa Ufaransa mabao 2-1 katika mchezo wa pili wa nusu fainali na kujikatia tiketi ya fainali ya michuano ya kombe la Ulaya upande wa wanawake itayapigwa Jumapili katika uwanja wa Wembley.

 

 

–

 

Nahodha wa timu ya Ujerumani na mshambuliaji machachari Alexandra Popp ndiye amepeleka kilio kwa timu ya Ufaransa kwa kufunga bao mbili katika kipindi cha kwanza na cha pili.

 

–

 

Popp aliitanguliza mbele Ujerumani kwa kufunga bao la kwanza mnamo dakika ya 40, lakini Ufaransa walisawazisha dakika nne baadae kwa bao zuri la Kadidiatou Diani. Bao la pili liliwekwa wavuni mano dakika ya 76 na kumfanya Popp kufikisha goli sita katika mechi tano.

 

–

 

 

Ujerumani, ambao ni mabingwa mara nane wa michuano hiyo ya Ulaya upande wa wanawake sasa itavaana na wenyeji England ambao walitinga fainali baada ya kuitandika Sweden bao 4-0 katika mchezo wa Jumanne. Fainali za michuano hiyo itashuhudiwa na mashabiki wapatao elfu 87,000 katika uwanja wa Wembley.

 

 

–

 

Ufaransa walikuwa na nafasi kubwa baada ya kipindi cha mapumziko na kutoa ushindani mkali kwa safu ya mashambulizi ya Ujerumani, lakini hata hivyo jitihada zao hazikuweza kuzaa bao. Kocha wa Ufaransa Corinne Diacre alisema kuwa “kwa bahati mbaya hatukufanya vyema usiku wa leo. Hatukuweza kuboresha nafasi za mabao tulizopata.”

 

 

ADVERTISEMENT

–

 

 

Naye kocha wa timu ya Ujerumani Martina Voss-Tecklenburg amesema mchezo wa fainali dhidi ya England utakuwa wa kiwango cha juu. “Tunajua watakuwa mbele ya mashabiki wengi wa nyumbani lakini tuko tayari kuwakabili”

 

–

ADVERTISEMENT

 

Kutinga fainali kwa Ujerumani ni mafanikio makubwa kwa nahodha wa timu hiyo Alexandra Popp ambaye anaichezea klabu ya Wolfsburg baada ya kukosa michuano miwili iliyopita kutokana na majeraha. Mwaka 2013 Popp aliweka rehani nafasi yake ya kushinda taji akiwa na timu ya taifa wakati alipocheza kutokana na jeraha la kifundo cha mguu na kuisaidia Wolfsburg kushinda mataji matatu msimu wa 2012-13.

 

–

 

Siku ya Jumapili, mshambuliaji huyo hatakuwa tu akipigania taji hilo bali pia kiatu cha dhahabu akiwa amejiunga na Beth Mead wa England wakiwa kileleni mwa orodha ya wafungaji wenye mabao mengi katika michuano hiyo. Wachezaji hao wawili wamevunja rekodi ya mchezaji wa Ujerumani Inka Grings kwa kufikisha mabao sita katika michuano ya kombe la Ulaya kwa wanawake mwaka 2009. Tofauti na Ujerumani ambao wamebeba kombe hilo mara nane, timu ya wanawake ya Ufaransa imeingia hatua ya nusu fainali kwa mara ya kwanza.

Related

ADVERTISEMENT
Shabani Rapwi

Shabani Rapwi

Shabani Rapwi (Kijana Mchapa Kazi) WhatsApp; 0689232546 Email ;shabanimohamed932@gmail.com

Related Posts

Mkazi wa Mufindi -Iringa akabidhiwa gari mpya Suzuki S Presso baada ya kuibuka mshindi promosheni ya Vodacom Tusua Mapene
BIASHARA

Mkazi wa Mufindi -Iringa akabidhiwa gari mpya Suzuki S Presso baada ya kuibuka mshindi promosheni ya Vodacom Tusua Mapene

by I am Krantz
Aug 13, 2022
Rais Samia Akiwa katika Ziara yake Mkoani Iringa 2022
HABARI

Rais Samia Akiwa katika Ziara yake Mkoani Iringa 2022

by ALFRED MTEWELE
Aug 12, 2022
BIL.11 kupelekwa Mafinga kuboresha miundombinu ya Mji
HABARI

BIL.11 kupelekwa Mafinga kuboresha miundombinu ya Mji

by ALFRED MTEWELE
Aug 12, 2022
Dkt. Mpango Aitaka NEMC na STAMICO Kufanya Tathimini Migodini
HABARI

Dkt. Mpango Aitaka NEMC na STAMICO Kufanya Tathimini Migodini

by ALFRED MTEWELE
Aug 12, 2022
Benki ya NMB yang’ara maonyesho ya Nanenane Mkoani Mbeya.
BIASHARA

Benki ya NMB yang’ara maonyesho ya Nanenane Mkoani Mbeya.

by I am Krantz
Aug 12, 2022
Rais Samia Akamilisha Ziara yake Mkoani Njombe
HABARI

Rais Samia Akamilisha Ziara yake Mkoani Njombe

by ALFRED MTEWELE
Aug 11, 2022

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
July 2022
M T W T F S S
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031
« Jun   Aug »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In