BEKI wa kimataifa kutoka Ivory Coast aliyetemwa na Simba, Pascal Wawa amerejea nchini na kutua Singida Big Stars baada ya kocha wa timu hiyo, Hans Pluijm kumvuta ili aitumikie kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
–
Wawa aliyeitumikia Simba kwa misimu minne tangu 2018 akitokea Al-Merrikh ya Sudan aliachana na timu hiyo Juni 23 mwaka huu kwa kuagwa kwa heshima katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa dhidi ya Mtibwa Sugar.
–
Taarifa za kuaminika kutoka Singida Big Stars ilieleza nyota huyo kujiunga na timu hiyo, likiwa ni pendekezo la kocha Pluijm na msaidizi wake, Mathias Lule aliyekuwa akiifundisha Mbeya City.