Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amevitaka vilabu vya michezo kufanya uwekezaji ikiwa ni pamoja na kujenga miundombinu ili kuinua michezo.
–
Mhe. Mchengerwa ametoa kauli hiyo kwenye usiku wa utoaji wa Tuzo za Mashindano ya NBC ya Shirikisho la soka nchini 2022 katika Hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam.
–
Waziri Mchengerwa amesisitiza kuwa wakati umefika wa Vilabu vya Tanzania kumiliki viwanja vyao kama vilabu vingine duniani ambapo ameliagiza Baraza la Michezo la Taifa(BMT) na Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kuratibu kikao baina yake na viongozi wa vilabu mapema juma lijalo ili kujadili utekelezaji wa suala hilo.
–
Aidha, amewataka viongozi wa vilabu kuzingatia maadili na kuachana na vitendo vya ukiukaji wa maadali ambapo amefafanua kwamba vilabu haviwezi kupiga hatua katika michezo endapo havitazingatia suala hilo. ” Wenzetu wanafanikiwa sana kwenye michezo kwa kuwa wanazingatia maadili” ameongeza, Mhe. Mchengerwa Amelitaka BMT kuchukua hatua kali kwa yoyote atakaye bainika kuvunja maadili.