Waziri Mkuu wa zamani wa Japan Shinzo Abe ameanguka baada ya kupigwa risasi katika hafla moja mjini Nara
–
Bw Abe alipigwa risasi mara mbili, huku risasi ya pili ikimpiga mgongoni na kumfanya aanguke chini. Ripoti zinasema kuwa mtu aliyefanya shambulio hilo amekamatwa.
–
Video zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii, ambazo hazikuweza kuthibitishwa, zinaonekana kuonyesha wahudumu wa afya wakiwa wamemzunguka Bw Abe katikati ya barabara, lakini sasa ameripotiwa kukimbizwa hospitalini.