Uongozi wa klabu ya Yanga umetoa taarifa baada ya kufungiwa kwa Msemaji wao, Haji Manara kwa miaka miwili kutojihusisha na soka pamoja na faini ya Sh20 milioni baada ya kukutwa na hatia ya kumtolea maneno yasiyofaa Rais wa TFF, Wallace Karia.
–
Klabu hiyo wanasikitishwa na adhabu hiyo huku ikiamini msemaji wao hakutendewa haki kwa sababu adhabu yake ni kubwa. Hivyo klabu ya Yanga ipo tayari kumuunga mkono Manara kutafuta haki zaidi.