Mtandao wa YouTube umetangaza kuondoa maudhui yote yanayohamasisha utoaji mimba usio salama.
–
Uamuzi huo umefikiwa kutokana na mahitaji ya taarifa hizo kuwa makubwa baada ya nchi nyingi ikiwemo Marekani kufuta sheria iliyokua ikiruhusu utoaji mimba.
–
Video zitakazofutwa ni pamoja na zenye taarifa za uongo kuhusu utoaji mimba na pia zitajumuishwa kwenye sera za upotoshaji.
–
YouTube imesema zoezi la kuondoa maudhui yanayoshauri na kutangaza mbinu zisizo salama za utoaji mimba limeanza wiki hii na litakuwa endelevu.