Afisa mipango miji wa Halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi Bw Dickson Beno Mwenda (37) anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumbaka binti Mdogo mwenye umri wa miaka 15 ndani ya gari.
–
Kamanda was polisi akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake amesema mtuhumiwa alikabidhiwa watoto wawili na mama yao ambaye walikuwa wanakunywa pombe pamoja BAR awapeleke nyumbani ndipo alipofika njiani alipaki gari lake pembeni na kutekeleza unyama huo.
–
Akiendelea kutoa taarifa Kamanda amesema kwa mahojiano ya awali amekiri kosa na Leo hii baada ya uchunguzi kukamilika anafikishwa mahakamani.
–
Pia jeshi la polisi limefanikiwa kumnasa na kumkuta na Mali za wizi Bwana John Gaudensi ambaye alivunja nyumbani kwa mwalimu Kenani Kasekwa na ni karani wa sensa na kuiba kishikwambi Cha sensa ,radio ,simu na pesa taslim sh 760,000 vyenye jumla ya thamani ya sh milioni moja laki tatu na elfu ishirini.