ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Monday, March 20, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

BENKI YA CRDB YASHIRIKI MAONESHO YA NANENANE KITAIFA, JIJINI MBEYA

I am Krantz by I am Krantz
Aug 2, 2022
in BIASHARA, HABARI
0
BENKI YA CRDB YASHIRIKI MAONESHO YA NANENANE KITAIFA, JIJINI MBEYA
0
SHARES
169
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

RelatedPosts

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AIPONGEZA BENKI YA CRDB, AHITIMISHA MAONESHO YA NANENANE JIJINI MBEYA

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AIPONGEZA BENKI YA CRDB, AHITIMISHA MAONESHO YA NANENANE JIJINI MBEYA

Aug 9, 2022

WAZIRI MBARAWA AWATAKA WAKANDARASI NA WAZABUNI KUCHANGAMKIA FURSA ZA UWEZESHAJI KUTOKA BENKI YA CRDB

Jul 21, 2022

Benki Ya CRDB Na IFC Kuongeza Upatikanaji Wa Mitaji Kwa Wajasiriamali Nchini Tanzania Na Burundi

Jul 12, 2022
Load More

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango (kushoto) akipata maelezo kuhusu huduma za uwezeshaji sekta ya kilimo zinazotolewa na Benki ya CRDB kutoka kwa Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Kilimo Biashara wa Benki ya CRDB, Maregesi Shaaban (kulia), wakati alipotembelea banda la Benki hiyo katika katika ufunguzi wa Maonesho ya Nanenane, yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya. Katikati ni Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Nyanda za juu kusini, Jeniffer Tondi akati akimpatia maelezo kuhusu huduma za uwezeshaji sekta ya kilimo zinazotolewa na Benki ya CRDB, wakati alipotembelea banda la Benki hiyo katika katika ufunguzi wa Maonesho ya Nanenane, yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya. Katikati ni Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango (kushoto) akizungumza na baadhi ya Viongozi wa Benki ya CRDB wakati alipotembelea banda la Benki hiyo katika katika ufunguzi wa Maonesho ya Nanenane, yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya. 
=======   =======   =======
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia, Dkt. Philip Mpango ameitaka Benki ya CRDB kupitia Umoja wa Mabenki Tanzania kutoa Elimu ya namna inavyotoa mikopo kwa wakulima ili waweze kuwa na uthubutu na kuleta tija  kwenye uzalishaji nchini.
Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Nanenane 2022 kitaifa yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya.
“Nachukua fursa hii kutaka Benki ya CRDB kupitia Umoja wa Mabenki Tanzania kutoa Elimu ya namna bora ya kutoa mikopo kwa wakulima ili waweze kuwa na uthubutu na kuleta tija kwenye uzalishaji nchini” alisema Dkt. Mpango.
Pia ametoa wito kwa vyama vyote vya ushirika nchini kujiunga na Benki ya CRDB ili viweze kujikwamua kiuchumi na kupata mazingira wezeshi katika sekta zote za kiuchumi.
Akielezea mchango wa Benki ya CRDB katika sekta ya kilimo nchini, Meneja Mwandamizi wa Benki ya CRDB Kitengo cha Kilimo Biashara, Maregesi Shaaban  alisema “Katika mwaka wa fedha wa 2021/22 Benki ya CRDB imetoa jumla ya mikopo ya kilimo inayofikia TZS. 769 Bilioni, sawa na asilimia 43% ya mikopo yote ya kilimo inayotolewa na mabenki hapa nchini.
Kati ya mikopo hiyo, TZS. 494 Bilioni imeelekezwa kwenye mazao makuu ya kimkakati hivyo kusaidia zaidi ya AMCOS 472 kupata mikopo kwa ajili ya kuongeza tija kwenye uzalishaji wa kilimo (mikopo ya pembejeo, maghala, ujenzi wa viwanda vya kuchakata mazao, mikopo kwa ajili ya miradi ya ufugaji, uwekezaji kwenye misitu na mazao yake pia uwekezaji kwenye uvuvi). Kwa kipindi cha miaka mitano ilyopita hadi kufikia mwezi Juni 2022, Benki ya CRDB imetoa mikopo kwenye sekta ya kilimo inayofikia kiasi cha TZS. 2.6 Trilioni”.
Benki ya CRDB ndio Benki pekee ya biashara iliyoanza kutoa  mikopo nafuu zaidi kwenye sekta ya kilimo kwa riba ya asilimia tisa (9%) tu kwa mwaka. Hali hii imechagiza uwekezaji kwenye sekta ya kilimo na hivyo kukuza uchumi wa nchi kupitia ajira na pato la taifa kwa ujumla.
Wakulima wadogo wadogo kupitia kwenye vyama vya Ushirika wanaunganishwa na mifumo madhubuti ya kifedha kupitia mtandao imara wa Benki ya CRDB. Mkulima anaweza kupata huduma za kifedha kupitia CRDB Wakala, simu za mkononi hivyo kujijengea tabia za kujiwekea akiba kupitia huduma rahisi zinazopatikana hadi vijijini.
Naye Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Jeniffer Tondi alimweleza Makamu wa Rais kuwa  Benki ya CRDB iko tayari kushirikiana na Serikali pamoja na wadau wengine wa sekta ya kilimo katika kuuimarisha ushirika. Tondi alisema Benki ya CRDB mpaka sasa imehusika katika kuzijengea uwezo benki mbili za ushirika  ambapo TZS. 3.2 Bilioni zilitolewa kwa TACOBA na TZS. 7.0 Bilioni kwa KCBL, hivyo kuwezesha Benki hizi za Ushirika kupata mtaji unaofikia kiasi cha TZS. 10.2 Bilioni
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

Related

Tags: CRDB
ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

RJ THE DJ VIFO VINAONGEZA MSONGO WA MAWAZO
HABARI

ROMY JONS AOMBA MSAMAHA

by Shabani Rapwi
Mar 20, 2023
MCHUNGAJI AFUNGA KANISA KISA ASHINDA MIL 100 ZA “KUBETI”
HABARI

MCHUNGAJI AFUNGA KANISA KISA ASHINDA MIL 100 ZA “KUBETI”

by ALFRED MTEWELE
Mar 20, 2023
WAZIRI BITEKO ATAKA BAJETI YA 2023/24 KUZINGATIA VIPAUMBELE VYA WIZARA
HABARI

WAZIRI BITEKO ATAKA BAJETI YA 2023/24 KUZINGATIA VIPAUMBELE VYA WIZARA

by Shabani Rapwi
Mar 20, 2023
TMA YATOA TAHADHARI MVUA KUBWA MIKOA HII KUANZIA LEO NA KESHO
HABARI

TMA YATOA TAHADHARI MVUA KUBWA MIKOA HII KUANZIA LEO NA KESHO

by Shabani Rapwi
Mar 20, 2023
WATU 5 WASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA WIZI MAFUTA SGR
HABARI

WATU 5 WASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA WIZI MAFUTA SGR

by ALFRED MTEWELE
Mar 20, 2023
MARUFUKU KUTOA FEDHA UPATE DHAMANA POLISI
HABARI

MARUFUKU KUTOA FEDHA UPATE DHAMANA POLISI

by Shabani Rapwi
Mar 20, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
August 2022
M T W T F S S
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031  
« Jul   Sep »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In