ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Saturday, June 10, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

Benki ya NBC yadhamini Kampeni ya ‘Uzazi ni Maisha Wogging’ kwa Uzazi Salama Zanzibar

I am Krantz by I am Krantz
Aug 28, 2022
in BIASHARA, HABARI
0
Benki ya NBC yadhamini Kampeni ya ‘Uzazi ni Maisha Wogging’ kwa Uzazi Salama Zanzibar
0
SHARES
53
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

RelatedPosts

BENKI YA NBC YAZINDUA KAMPENI MPYA YA SHINDA MECHI ZAKO NA NBC

BENKI YA NBC YAZINDUA KAMPENI MPYA YA SHINDA MECHI ZAKO NA NBC

May 3, 2023

HUDUMA YA NBC CONNECT YAZINDULIWA MBEYA ,KUBORESHA HUDUMA ZA KIBENKI MKOANI HUMO

May 1, 2023

NAFASI ZA KAZI BENKI YA NBC

Apr 25, 2023
Load More

A

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akianzisha Mbio fupi za kilomita 10 pamoja na matembezi ya kilomita 5 kuanzia viwanja wa Maisara Suleiman Jijini Zanzibar mpaka Uwanja wa Amaan Studium,zilizoandaliwa na Shirika  la AMREF HEALTH AFRICA na kudhaminiwa na Benki ya Biashara ya Taifa  NBC  ,ambapo Viongozi mbali mbali wameshiriki katika matembezi hayo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (katikati) akiongoza matembezi ya kilomita 5 yaliyofayika leo kuanzia viwanja wa Maisara Suleiman Jijini Zanzibar hadi uwanja wa Amaan Studium ikiwa ni kampeni ya “Uzazi ni Maisha”yaliyoandaliwa na Shirika  la AMREF HEALTH AFRICA na kudhaminiwa na Benki ya NBC  ,ambapo Viongozi mbali mbali matembezi hayo .

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (katikati) akiongoza matembezi ya kilomita 5 yaliyofayika leo kuanzia viwanja wa Maisara Suleiman Jijini Zanzibar hadi uwanja wa Amaan Studium ikiwa ni kampeni ya “Uzazi ni Maisha”yaliyoandaliwa na Shirika  la AMREF HEALTH AFRICA  na kudhaminiwa na Benki ya NBC ,ambapo Viongozi mbali mbali matembezi hayo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk Hussein Mwinyi akimkabidhi cheti cha pongezi Mkurungezi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw.Theobald Sabi hapo jana ambapo @nbc_tanzania walidhamini matembezi ya ya ‘Uzazi ni Maisha Wogging Marathon’ kwa kushirikiana na shirika la Amref Health Africa Tanzania na Wizara ya Afya ya Zanzibar ampeni ya “Uzazi ni Maisha ambayo imejumuisha wanamichezo mbali mbali kwa matembezi ya kilomita 5 pamoja na mbio fupi za kilomita 10 kuanzia viwanja wa Maisara Suleiman Jijini Zanzibar mpaka Uwanja wa Amaan Studium
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa MkurungezI mtendaji wa Benki ya NBC Bw; Theobald Sabi wakati alipotembelea katika maonesho ya kazi na huduma mbali mbali zinazotolewa na Benki hiyo katika hafla ya Kuchangia Kampeni ya “Uzazi ni Maisha ambayo imejumuisha wanamichezo mbali mbali kwa matembezi ya kilomita 5 pamoja na mbio fupi za kilomita 10 kuanzia viwanja wa Maisara Suleiman Jijini Zanzibar mpaka Uwanja wa Amaan Studium,zilizoandaliwa na Jumuiya ya AMREF HEALTH AFRICA na kudhamimiwa na Benki ya NBC .

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akipokea zawadi maalum kutoka kwa Mkurugenzi Mkaazi wa AMREF HEALTH AFRICA Dr. Florence Temu katika hafla ya Kuchangia Kampeni ya “Uzazi ni Maisha ambayo imejumuisha wanamichezo mbali mbali ka matembezi ya kilomita 5 pamoja na mbio fupi za kilomita 10 kuanzia viwanja wa Maisara Suleiman Jijini Zanzibar mpaka Uwanja wa Amaan Studium,zilizoandaliwa na Jumuiya ya AMREF HEALTH AFRICA ,ambapo Viongozi mbali mbali wameshiriki katika matembezi hayo. 

 

Zanzibar, Tanzania – 27 Agosti, 2022 – Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Shirika la Amref Health Africa Tanzania, na Wizara ya Afya ya Zanzibar, leo imeendesha kampeni ya ‘Uzazi ni Maisha Wogging Marathon’ katika Uwanja wa Sheikh Amani, Zanzibar, Tanzania.

Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Dr. Hussein Ali Mwinyi, alikuwa ndiye Mgeni Rasmi wa tukio hilo la Matembezi, Mbio Fupi na Ndefu (Wogging (Walk-Jog-Run)).
Kwa kauli mbiu: “Changia Vifaa Tiba kwa Uzazi Salama” matembezi, mbio fupi na ndefu (kwa kifupi ‘wogging’) zilizopata umaarufu zilikazia kutoa elimu kuhusu upungufu uliopo katika sekta ya afya na kukusanya fedha ili kusaidia jitihada za serikali katika kuhakikisha kwamba vifaa tiba na dawa kwa uzazi salama vinapatikana katika vituo vya afya vilivyobainishwa hapa Zanzibar. Kwa hiyo, tukio hilo lililolenga kuhamasisha taasisi za umma, makampuni na sekta binafsi, watu binafsi pamoja na wadau wengine kuchangia na kutoa msaada wa vifaa tiba na dawa kwa uzazi salama Visiwani.

Kampeni hiyo iliwawaleta pamoja zaidi ya washiriki 4,000 ambao ni pamojana maofisa wa ngazi za juu wa makampuni, wanadiplomasia, washirika wa maendeleo, maofisa wa serikali, vyombo vya habari na watu binafsi ambao waliotoa ahadi na kueleza utayari wao wa kusaidia kuchangia kampeni hii kupitia njia mbalimbali za utoaji msaada.
Katika kipindi cha miaka mitatu, Kampeni ya Uzazi ni Maisha Wogging inalenga kukusanya zaidi ya Shilingi za Tanzania bilioni moja ikiwemo misaada ya vitu, fedha taslimu na ahadi za kutoa misaada ya vifaa tiba kwa uzazi salama. Kampeni itaendeshwa kwa miaka mitatu huku kukiwa na ushiriki wa wadau mbalimbali hadi hapo lengo litakapofikiwa.
Mgeni rasmi wa tukio hili, Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, alipongeza juhudi za Amref kwa kubuni njia hiyo ya kipekee na kuwaasa wadau zaidi kushiriki ili kuhakikisha wanakuwa sehemu ya upatikanaji wa vifaa tiba na dawa kwa ajili ya uzazi salama hapa Zanzibar. Alisema michango hiyo mikubwa ni muhimu sana na msaada utakaotolewa utaelekezwa katika kuokoa maisha ya kina mama na watoto wachanga, na hivyo kupunguza vifo wakati wa uzazi, ambavyo vinaweza kuzuiwa hapa nchini.
“Idadi ya vifo vinavyotokana na matatizo ya uzazi vinavyowaathiri moja kwa moja akina mama na watoto wachanga bado iko juu hapa Zanzibar, ikiwa ni vifo vya akinamama 267 kati ya vizazi hai 100,000 kwa mwaka; na wastani wa vifo 28 vya watoto kati ya vizazi hai 1,000 kwa watoto wachanga (kutokana na takwimu za HMIS 2017). Huduma za mama na mtoto katika vituo vyetu vya afya zina changamoto nyingi ambazo zinachangia katika vifo hivi vitokanavyo na matatizo ya uzazi ikiwemo upungufu wa vifaa tiba, dawa na uhaba wa wahudumu wa afya. Nimetaarifiwa, Kupitia kampeni hii ya Uzazi ni Maisha, jumla ya vituo vya afya 28 vitapata vifaa tiba ambayo ni sawa na asilimia 40.5% ya vituo vyote vinavyotoa huduma ya mama na mtoto katika vijiji vilivyo hapa Zanzibar. Namhimiza kila mmoja ajitahidi kuwa sehemu ya mpango huu mwema na kuleta mafaniko kwa Serikali yetu ya Zanzibar,” alisema Mh. Mwinyi.

Vile vile, Dkt. Mwinyi aliipongeza Benki ya NBC kwa kushirikiana na Amref Tanzania na kusaidia kampeni hiyo muhimu kwa kushirikiana na serikali ili kupunguza idadi vya vifo vya akina mama hapa Zanzibar.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, akitoa hotuba yake alisisitiza kuwa wana dhamira kubwa ya kuboresha afya ya Mama na Mtoto “Benki ya NBC pia tunaunga mkono ajenda ya taifa ya kuboresha Afya ya mama na mtoto kupitia msaada wa Kliniki za Magari yaani (Mobile Clinic Vans) ambazo tumezitoa kwa serikali kupitia halmashauri za miji ya Unguja-Zanzibar na Dar es Salaam.

.

ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

Related

Tags: NBC
ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA POLE KWA FAMILIA YA MMILIKI WA PRECISION AIR
HABARI

RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA POLE KWA FAMILIA YA MMILIKI WA PRECISION AIR

by ALFRED MTEWELE
Jun 10, 2023
BREAKING; MMILIKI WA PRECISION AIR AFARIKI DUNIA
HABARI

BREAKING; MMILIKI WA PRECISION AIR AFARIKI DUNIA

by ALFRED MTEWELE
Jun 10, 2023
YALIYOJIRI KWENYE MAGAZETI YA LEO JUNI 10, 2023
HABARI

YALIYOJIRI KWENYE MAGAZETI YA LEO JUNI 10, 2023

by ALFRED MTEWELE
Jun 10, 2023
Benki ya NBC yakabidhi kombe la ubingwa wa ligi kuu kwa Yanga
HABARI

Benki ya NBC yakabidhi kombe la ubingwa wa ligi kuu kwa Yanga

by I am Krantz
Jun 10, 2023
Relationship Manager; Mass Affluent (Acquisition) Job Vacancy at NMB Bank PLC
HABARI

Relationship Manager; Mass Affluent (Acquisition) Job Vacancy at NMB Bank PLC

by ALFRED MTEWELE
Jun 9, 2023
Application Support Specialist Job Vacancy at NBC
HABARI

Application Support Specialist Job Vacancy at NBC

by ALFRED MTEWELE
Jun 9, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
August 2022
M T W T F S S
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031  
« Jul   Sep »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In