Benki ya CRDB katika kuonesha dhamira ya upekee katika ubunifu ndani ya soko lake imeamua kuongeza mbio za baiskeli zenye umbali wa kilometa 65 ndani ya CRDB Marathon msimu wa 3 itakayofanyika Agosti 14, 2022. Zaidi ya hapo wameambatanisha na zawadi ya fedha taslimu washindi 1-6 watakazojinyakulia zikitolewa hapo baadae ndani ya jengo la Johari Rotana, Posta.