
Rais wa Serikari kuu ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi ameipongeza Benki ya NBC pamoja na Amref Tanzania kwa kusaidia kampeni ya kuchangia vifaatiba kwa uzazi salama kwa kushirikiana na Serikali ili kupunguza idadi vya vifo vya akina mama Zanzibar.
Vile vile Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, akitoa hotuba yake alisisitiza kuwa tuna dhamira kubwa ya kuboresha afya ya Mama na Mtoto. Benki ya NBC pia tunaunga mkono ajenda ya taifa ya kuboresha Afya ya mama na mtoto kupitia msaada wa Kliniki za Magari yaani (Mobile Clinic Vans) ambazo tumezitoa kwa Serikali kupitia halmashauri za miji ya Unguja-Zanzibar na Dar es Salaam.
Kupitia Kliniki hizi, ambazo zilianzishwa mwaka 2020, tumefanikiwa kuwafikia jumla ya walengwa milioni tatu ambapo huduma zote hutolewa BURE. Gari jipya la Kliniki hizi tulilolitoa hapa Zanzibar mwaka 2021 limefanikisha kuwahudumia wakinamama na watoto zaidi ya milioni moja na nusu na hivyo kusaidia sana kupunguza vifo vya kinamama wakati wa kujifungua (Maternal Deaths).
ADVERTISEMENT