Kwa hapa Tanzania wanawake wengi wanaovaa kipini puani ni wale wa Pwani, na wengi wanaotoboa pua hutoboa zaidi upande wa kushoto. Baadhi ya makala zilizoandikwa kuhusu utoboaji wa upande wa kushoto wa pua zinasema yafuatayo;
• Hupunguza maumivu ya tumbo wakati wa hedhi na kusawazisha hedhi zisizo na mpangilio.
• Husaidia kuimarisha afya ya mfumo wa uzazi
• Hupunguza maumivu wakati wa kujifungua.
• Hupunguza maumivu ya kipandauso.
• Huboresha viungo vya uzazi.
Tovuti ya onmanorama inaelezea kuwa zipo neva zinazohusiana na mfumo wa uzazi ambazo huishia kwenye pua, hivyo kutoboa pua huziamsha neva hizo kufanya kazi bora zaidi.