Mwanamke mmoja nchini Saudi Arabia amehukumiwa kifungo cha miaka 45 jela kutokana na posti zake za kwenye mitandao ya kijamii.
Mahakama ya ugaidi imemtia hatiani Nourah bint Saeed al-Qahtani kwa kuvunja maadili ya jamii na kukiuka taratibu za umma kwa kutumia mitandao ya kijamii.
Hakuna taarifa nyingi zinazojulikana kumhusu Nourah zaidi ya kuwa alikuwa akipigania haki za wanawake na kuwakosoa viongozi wa Saudi.
Tangu mwaka jana, wanaharakati wengi wa kike nchini humo wamekamatwa kutokana na posti zao za mitandaoni.
Tarehe 9 mwezi uliopita mwanamke mwingine alihukumiwa kifungo cha miaka 34 jela kwa matendo yake kwenye mtandao wa Twitter.