Karani wa Sensa kata ya Majimoto Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe mkoani Katavi, Kenan Kasekwa amevamiwa usiku wa kuamkia leo na kuporwa kishikwambi (tablet) cha Sensa na fedha taslimu sh 760,000/=.
–
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpimbwe Catherine Mashala amesema Karani aliyevamiwa ni mwalimu na alivamiwa na mtu ambaye alivunja kitasa na kuingia chumbani kwake baada ya kumpulizia kinachodhaniwa ni dawa ya usingizi.
–
Hata hivyo tayari Jeshi la Polisi limeshafanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa uhalifu huo.