Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula amepokea gari aina ya “Landcruiser Hardtop” kutoka Shirika la Pact Tanzania kupitia mradi wa Achieve (unaofadhiliwa na USAID) kwa lengo la kuimarisha huduma mbalimbali za Ustawi wa Jamii hasa Makundi ya watoto wanaoishi mazingira magumu na Wazee. Gari hiyo ina thamani ya zaidi shillingi millioni 80. Katika mapokezi hayo alizungumza mengi na kutoa rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi zima la SENSA ili waweze kuhesabiwa kwa maendeleo ya wote.