“Hakuna anaeweza kujificha kwa kusema ni kawaida ya mpira, mateso hayapaswi kuwa kawaida
Ukweli ni kwamba tunapitia maumivu makali mnoo, kila mwanasimba leo anaugua kivyake.
–
Poleni sana ndugu zangu hakuna neno la kufuta machungu yenu Mlichokitegemea sicho mlichopata inaumiza sana, kila nikitazama macho ya Wanasimba naona uchungu na maumivu yaliyopitiliza.
–
Tumeshapoteza, tutulie tone tunaingiaje msimu mpya, Sio rahisi kusahau lakini tunapaswa kujisahaulisha maana ligi inaanza wiki ijayo ni muhimu zaidi kuanza vizuri. Panapovuia pameonekana tuwaachie wahusika wafanye maamuzi sahihi,” Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba Sc, Ahmed Ally