ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Monday, February 6, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

LIFAHAMU ZAIDI JIJI LA DAR ES SALAAM

Dar es Salaam, Tanzania

ALFRED MTEWELE by ALFRED MTEWELE
Aug 25, 2022
in HABARI
0
LIFAHAMU ZAIDI JIJI LA DAR ES SALAAM
0
SHARES
135
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

millardayo on Twitter: "Muonekano wa jiji la Dar es salaam, Tanzania leo  March 2, 2017 https://t.co/QRVw16XuVT" / Twitter

Jiji la Dar es Salaam lipo kati ya Latitudo nyuzi 6 hadi 7 na Longitudo kati 39.45 kwa upande wa Mashariki na nyuzi 39 kwa upande wa Magharibi, Kusini mwa Ikweta na upande wa Magharibi, Kusini na Kaskazini. Jiji linapakana na Mkoa wa Pwani, upande wa Mashariki linapakana na Bahari ya Hindi, ambapo kuna ufukwe wenye urefu wa km. 124 unaoanzia Pemba Mnazi hadi Mbweni.

RelatedPosts

No Content Available
Load More

Jiji la Dar es Salaam lina eneo la ukubwa wa kilomita za Mraba zipatazo 1,800; kati ya hizo, kilomita za mraba 1,350 ni eneo la nchi kavu ikijumuisha visiwa vinane vilivyopo katika eneo la bahari ya Hindi na kilomita za mraba 450 ni eneo la maji ya bahari. Eneo la Jiji la Dar es Salaam ni sawa na asilimia 0.2 ya eneo la nchi nzima ambalo ni kilomita za mraba 881,289.

Hali ya Hewa

Jiji hili lina hali ya hewa ya Joto ya Pwani ya Tropical, likiwa na wastani wa nyuzi joto 25 hadi 33 sentigredi na wastani wa mvua wa mililita 1,000 katika misimu miwili ya vuli ambayo ni miezi ya Oktoba – Desemba na Masika ambayo huanza miezi ya Machi – Mei. Wakati mwingi Jiji hutawaliwa na pepo zivumazo toka baharini zikitokea Kusini, Mashariki na Kaskazini mwa Bahari ya Hindi.

Idadi ya watu

Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 Jiji lina idadi ya watu 4,364,541, ambapo kati yao wanaume ni 2,125,786 na wanawake ni 2,238,755. Aidha, idadi ya watu imekua ikiongezeka kwa wastani wa asilimia 5.6 kwa mwaka. Wastani wa watu kwa kila kilomita moja ya mraba ilikuwa ni 3,137 na ukubwa wa Kaya ni wastani wa watu 4 kwa Kaya. Kwa ongezeko hilo la watu kwa mwaka, Jiji la Dar es Salaam mwaka 2018 linakadiriwa kuwa na idadi ya watu 6,107,473. Idadi hii ya watu inaongeza msongamano wa watu wanaokadiriwa kuwa 4,383 kwa kila kilometa moja ya mraba.

Historia ya Halmashauri ya Jiji

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imekuwa inaliongoza Jiji kutoka mwaka 1961 mpaka mwaka 1972, ambapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilizivunja Halmashauri zote nchini na kuwa chini ya Usimamizi wa Serikali Kuu (Madaraka Mikoani)

Serikali Kuu ilizirudisha Serikali za Mitaa Nchini, Chini ya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) na. 8 ya mwaka 1982, ambapo Halmashauri ya Jiji ilianza kutekeleza majukumu yake ya kutoa huduma kwa wananchi kuanzia mwaka 1983.

Mwaka 1996 Serikali Kuu iliivunja Halmashauri ya Jiji na kuunda Tume ya Jiji la Dar es Salaam, kwa Tangazo la Serikali Na. 110 na 111 ya tarehe 28 Juni mwaka 1996.

Tume ya Jiji ilifanya kazi kwa kipindi cha miaka minne, ambapo mwaka 2000 Serikali iliunda mamlaka nne za Serikali za Mitaa za Mkoa wa Dar es Salaam kwa sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Na. 8 ya Mwaka 1982, kama ilivyo rekebishwa kwa sheria na. 6 ya mwaka 1999.

Utawala

ADVERTISEMENT

Kiutawala Jiji limegawanyika katika Halmashauri sita za Serikali za mitaa ambazo ni:

  • Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam
  • Halmashauri ya Manispaa ya Temeke
  • Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni
  • Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
  • Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo na
  • Halmashauri ya Manispaa ya KigamboniLocal

ADVERTISEMENT

Muundo

Halmashauri ya Jiji inaundwa na Baraza la Madiwani, Idara tano na Vitengo vinne.

Baraza la Madiwani

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam linaundwa na Madiwani 26 kutoka katika Manispaa tano za Jiji la Dar es Salaam na linawakilishwa na Wajumbe wafuatao: Mameya 5, Madiwani 16 na Wabunge 5.

Mstahiki Meya wa Jiji ni Kiongozi Mkuu na Mkurugenzi wa Jiji ni Mtendaji Mkuu kwa upande wa Serikali za Mitaa. 

Majukumu ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam iliundwa na kupewa majukumu ya kuratibu na kusimamia shughuli za uendelezaji wa Jiji katika Halmashauri za Manispaa zote tatu. Majukumu hayo ni kwa mujibu wa Sheria za serikali za mitaa (Mamlaka za Miji) Na.8 ya mwaka 1982 kifungu cha 69A kama ilivyorekebishwa na sheria Na.6 ya mwaka 1999.

Majukumu hayo ni kama ifuatavyo:

  • Kuratibu Mamlaka na wajibu wa kila Halmashauri za Manispaa juu ya miundombinu na matumizi bora ya ardhi.
  • Kuandaa Mpango Mkakati kwa ajili yakuhakikisha kuwa panakuwepo na maendeleo endelevu ya Jiji
  • Kukuza ushirikiano kati ya Mamlaka za Halmashauri zote zilizopo katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
  • Kushughulikia masula yote yanayohusu ushirikiano kati ya Malmaka za Serikali za Mitaa zilizopo katika Jiji la Dar es Salaam.
  • Kuhakikisha panakuwepo amani na utulivu pamoja na kutoa msaada katika huduma kama vile Zimamaoto na maokozi, Polisi na magari ya kubeba wagonjwa.
  • Kutekeleza majukumu mengine yoyote kama itakavyokubalika na Halmashauri nyingine zilizopo.
  • Kutekeleza majukumu ya itifaki na sherehe za Kimkoa au /na Kitaifa.

Uboreshaji wa Muundo wa Jiji la Dar es Salaam kuwa mamlaka sita umeleta ufanisi mkubwa katika utoaji bora wa huduma kwa jamii kwani madaraka yamesogezwa karibu zaidi na wananchi.

HII NDIYO HISTORIA YA JIJI LA DAR ES SALAAM - YouTube

Related

Tags: Dar es Salaam
ADVERTISEMENT
ALFRED MTEWELE

ALFRED MTEWELE

Related Posts

DIAMOND KANILIPA MILIONI 17 VIDEO YA ZUWENA
HABARI

DIAMOND KANILIPA MILIONI 17 VIDEO YA ZUWENA

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
VIJANA ACHENI KU-BET FANYENI KAZI – CHONGOLO
HABARI

VIJANA ACHENI KU-BET FANYENI KAZI – CHONGOLO

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
RAIS WA ZAMANI WA PAKISTAN AFARIKI DUNIA
HABARI

RAIS WA ZAMANI WA PAKISTAN AFARIKI DUNIA

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
IDADI YA WALIOFARIKI AJALI YA TANGA YAONGEZEKA HADI 20
HABARI

IDADI YA WALIOFARIKI AJALI YA TANGA YAONGEZEKA HADI 20

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
MANGE KIMAMBI AMCHANA  HAJI MANARA ‘WE NI MTU MZIMA’
HABARI

MANGE KIMAMBI AMCHANA HAJI MANARA ‘WE NI MTU MZIMA’

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023
NAJUA UCHUNGU WA MTOTO SIWEZI – WOLPER
HABARI

NAJUA UCHUNGU WA MTOTO SIWEZI – WOLPER

by Shabani Rapwi
Feb 5, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
August 2022
M T W T F S S
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031  
« Jul   Sep »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In