USIKU wa kuamkia leo August 28, Bondia mtu kazi KARIM MANDONGA, ameibuka kidedea katika pambano la uzito wa kati kwa kumpiga Bondia SOTII MDUDU kutoka Kigoma kwa Technical Knockout (TKO) round ya 4 katika pambano la round 8.
–
Pambano hilo limechezwa Kigoma katika fukwe za Ziwa Tanganyika Kidyama huku Mashabiki wa Mchezo wa masumbwi mkoani Kigoma wakijitokeza kwa wingi kutazama pambano hilo.
–
Wikiendi iliyopita MANDONGA alishinda pambano lake kwa KO raundi ya kwanza. Septemba 24 atapanda ulingoni mkoani Mtwara katika pambano la Ubabe Ubabe 2.