Rapa Mr Blue Anasema kuwa yeye na Mke wake walikutana Club Bilicanas.
–
Mr blue akiwa kwenye Kipindi cha Kisofa cha #Etv Amesema kuwa alivyokuwa Ameenda Bilicanas kwa ajili ya kazi zake za Kimuziki ndipo alipokutana nae yeye akiwa kwenye Birthday ya Dada yake na Akampenda na kumtuma Baunsa kwenda kumuita Wakaongea.
–
“Mimi na Mke wangu ni kweli tumekutana Klabu Bilicanas Jumapili mchana yeye alikuwa ameenda kwenye Birthday ya Dada yake na mimi nilienda kwa ajili ya Kazi zangu za kimuziki hivyo nikampenda nikamtuma Baunsa akamuite, Nikaongea nae tukabadilishana namba na Sasa hivi ni Mke wangu,Mke mzuri sio lazima umpate tu Kanisani”