Kumekuwa na matukio ya makarani wa sensa kupiga picha wakiwa katika majukumu yao na picha hizo kusambaa katika mitandao ya kijamii, kumbe kufanya hivyo ni kosa.
–
Na kwa sababu hiyo, Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dk Albina Chuwa amesema adhabu anayostahili karani aliyefanya kosa la kupiga picha na kurekodi video wakati sensa ya watu na makazi ni faini ya Sh2 milioni, kifungo cha miezi sita au vyote kwa pamoja.
–
Mitandao ya kijamii imeshuhudia baadhi ya watu wakifanya hivyo wakati zoezi la sensa likiendelea. Amesema ni kinyume cha sheria kwa karani yeyote kufanya hivyo anapochukua taarifa za wananchi na kwamba waliofanya hivyo, watachukuliwa hatua.
–
Ameyasema hayo wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya Sensa ya Watu na Makazi Mkoani Iringa. “Ni kosa kurekodi au kujirekodi mnapokuwa katika majukumu yenu,” amesema.