Rais Samia Suluhu Hassan ameipongeza timu ya Simba Queens kwa kutwaa ubingwa wa CECAFA 2022 baada kuifunga timu ya She Corporate ya Uganda bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliopigwa usiku wa jana uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
–
Kupitia katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Rais Samia amesema kuwa Simba Queens imejenga heshima kwa Soka la Tanzania na kuwatakia kila la kheri katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake itakayofanyika Morocco.
–
“Nawapongeza wanangu Simba Qeens SC kwa ubingwa wa Afrika Mashariki wa CECAFA 2022 kwa Wanawake (SAMIA CUP). Mmejenga heshima kwa soka la Tanzania na nchi kwa ujumla. Nawatakia kheri katika Ligi ya Mabingwa Afrika (2022 CAF Women’s Champions League ) itakayofanyika nchini Morocco”