ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Tuesday, March 28, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AIPONGEZA BENKI YA CRDB, AHITIMISHA MAONESHO YA NANENANE JIJINI MBEYA

I am Krantz by I am Krantz
Aug 9, 2022
in BIASHARA, HABARI
0
RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AIPONGEZA BENKI YA CRDB, AHITIMISHA MAONESHO YA NANENANE JIJINI MBEYA
0
SHARES
120
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameipongeza Benki ya CRDB kwa kushirikiana na Serikali kubuni mfumo wa kidigitali utakaoiwezesha Wizaya ya Kilimo kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kuagiza mbolea na kuisambaza kwa mkulima, hivyo ruzuku itolewayo na Serikali kumfikia mnufaika kama ilivyokusudiwa.

Mhe. Rais ametoa pongezi hizo jana alipohitimisha rasmi Maonyesho ya wakulima Nanenane katika Viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.  Mhe. Rais amezitaka taasisi za fedha na benki za biashara nchini kuendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha sekta ya kilimo inapewa kipaumbele.

“Aidha, nazipongeza benki nchini kwa kushiriki vyema katika kuhakikisha sekta ya kilimo inakua na kuleta tija nchini, niipongeze Benki ya CRDB kwa kushirikiana na Serikali kufanikisha mfumo huu kwani naamini utaleta mapinduzi makubwa ya kilimo nchini,” alisema Rais Samia.

RelatedPosts

BENKI YA CRDB YASHIRIKI MAONESHO YA NANENANE KITAIFA, JIJINI MBEYA

BENKI YA CRDB YASHIRIKI MAONESHO YA NANENANE KITAIFA, JIJINI MBEYA

Aug 2, 2022

WAZIRI MBARAWA AWATAKA WAKANDARASI NA WAZABUNI KUCHANGAMKIA FURSA ZA UWEZESHAJI KUTOKA BENKI YA CRDB

Jul 21, 2022

Benki Ya CRDB Na IFC Kuongeza Upatikanaji Wa Mitaji Kwa Wajasiriamali Nchini Tanzania Na Burundi

Jul 12, 2022
Load More

Benki ya CRDB imekuwa kinara katika kuhakikisha inashirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wadau wa sekta za kilimo, uvuvi, mifugo, misitu, biashara na viwanda ikiongozwa na kaulimbiu yake isemayo “Kilimo chetu, Viwanda vyetu, Uchumi Wetu” hivyo kuongeza tija ya uwekezaji kwenye sekta hizo ikizingatiwa umuhimu wa kuunganisha wateja wote kwenye mnyororo wa thamani katika uzalishaji ili kuwapatia uhakika wa masoko ya bidhaa zao.

Mkurugenzi Mtendaji Abdulmajid wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alielezea namna benki hiyo ya kizalendo imekuwa mdau mkubwa wa sekta zote za kiuchumi nchini  kwa kuwasaidia wakulima, wafugaji au wavuvi iwe mmojammoja, vikundi, vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS), wakulima wakubwa, wafanyabiashara wa mazao ya kilimo na wawekezaji kwenye viwanda vinavyoongeza thamani ya malighafi zinazozalishwa nchini.  

“Kiujumla zaidi ya 43% ya mikopo yote itolewayo kwa ajili ya kilimo nchini imetolewa na Benki ya CRDB.  Kwa mwaka 2021/2022,  tumetoa zaidi ya shilingi bilioni 769. Sehemu kubwa ya mikopo itolewayo na Benki ya CRDB imeelekezwa katika kilimo cha mazao ya biashara, kilimo cha mazao ya chakula, uvuvi, mifugo, uzalishaji wa malighafi za viwanda, ujenzi wa viwanda vya  uchakataji wa mazao ya kilimo, utengenezaji wa pembejeo, uendelezaji wa mazao ya misitu, usindikaji na usambazaji,” alisema Nsekela.

Kwa kipindi cha miaka mitano ilyopita hadi Juni 2022, alisema Benki ya CRDB imetoa mikopo kwenye sekta ya kilimo kiasi cha TZS 2.6 Trilioni. Ikumbukwe CRDB ilikuwa benki ya kwanza nchini kutoa mikopo kwa riba ya tarakimu moja ikitoza asilimia 9 katika sekta ya kilimo.

Maeneo makubwa ambayo Benki ya CRDB imejikita katika kusaidia uwezeshaji kwenye sekta ya kilimo ni mikopo ya pembejeo na uendeshaji wa mashamba ambapo imesaidia upatikanaji wa mbolea na pembejeo nyinginezo muhimu kwa gharama nafuu. Sehemu kubwa ya mbolea inayoingizwa nchini inatokana na uwezeshaji wa CRDB.

Benki pia imebuni utaratibu mzuri wa kuagiza mbolea kupitia utaratibu mahususi wa dhamana (Letter of Credit) ambapo waagizaji wa mbolea huweza kuingiza bidhaa hii muhimu kwa kilimo kwa gharama nafuu ya asilimia 2 kwa mkopo wa fedha za kigeni na asilimia 4 kwa mwaka kwa mkopo wa shilingi za Kitanzania.

Awali, maonyesho hayo yaliyofunguliwa na Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Philip Mpango, alizitaka benki nchini kushirikiana na Serikali akisisitiza kuwa Benki ya CRDB inachukulia kwa umuhimu mkubwa kuziwezesha sekta muhimu zenye mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Taifa.

“Tunafahamu kuwa Serikali yetu ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wako Mheshimiwa Rais, imedhamiria kwa dhati kabisa, kujenga uchumi unaoshamirishwa na kilimo, uvuvi, mifugo, misitu, biashara na viwanda. Kiuhalisia sehemu kubwa ya viwanda vyetu vinategemea sana mazao ya kilimo, uvuvi na mifugo kama chanzo muhimu cha malighafi. Sisi Benki ya CRDB tupo mstari wa mbele kuunga mkono juhudi hizi kwa kutoa mazingira wezeshi ya upatikanaji wa fedha na elimu ya uwekezaji,” alisema Nsekela.

ADVERTISEMENT

Kwa mara ya kwanza, Serikali imetenga TZS. 150 bilioni kwa ajili ya ruzuku ya mbolea ili kupunguza gharama za pembejeo hii ni baada ya kutenga TZS. 1.0 Trilioni kuzipa benki nchini chanzo nafuu cha fedha kwa ajili ya mikopo nafuu kwenye kilimo.

Wateja wa Benki ya CRDB wanaweza kupata huduma za fedha kwa wakala wa CRDB, kwenye simu zao za mkononi au kwenye tawi la benki hata mashine za kutolea fedha zinazopatikana hadi vijijini.

Pamoja na jitihada hizo, Benki imeingiza sokoni akaunti maalum kwa ajili ya wakulima, wafugaji na wavuvi ijulikanayo kama “Fahari Kilimo” ikiwa ni sehemu ya mkakati mpana wa kuwahudumia wakulima kwa ukaribu kwa kuzingatia mahitaji yao. Nsekela amesema benki itaendelea kuwezesha zaidi ili kuinua uchumi wa Taifa kupitia fursa zilizopo kwenye sekta zote za uchumi.

ADVERTISEMENT

Related

Tags: CRDBSAMIA
ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

TAASISI YA GREEN KIDS AND YOUTH FOUNDATION  KUENDELEZA MAHUSIANO BORA NA WADAU KATIKA KUTETEA UNYANYASAJI WA KIJINSIA
HABARI

TAASISI YA GREEN KIDS AND YOUTH FOUNDATION KUENDELEZA MAHUSIANO BORA NA WADAU KATIKA KUTETEA UNYANYASAJI WA KIJINSIA

by Ally Hamis Zingizi
Mar 27, 2023
NALA kuwekeza zaidi ya Sh. Bilioni 2 baada ya kupata leseni ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT)
HABARI

NALA kuwekeza zaidi ya Sh. Bilioni 2 baada ya kupata leseni ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT)

by I am Krantz
Mar 27, 2023
Naibu Waziri   aipongeza Benki ya NBC kwa kusaidia maendeleo ya  michezo
HABARI

Naibu Waziri aipongeza Benki ya NBC kwa kusaidia maendeleo ya michezo

by I am Krantz
Mar 27, 2023
MZEE WA MIAKA 92 AFUNGA NDOA YA TANO MWAKA MMOJA BAADA YA NDOA NNE KUVUNJIKA
HABARI

MZEE WA MIAKA 92 AFUNGA NDOA YA TANO MWAKA MMOJA BAADA YA NDOA NNE KUVUNJIKA

by Shabani Rapwi
Mar 27, 2023
BAKWATA YASHIKILIA MSIMAMO NDOA MIAKA 14
HABARI

BAKWATA YASHIKILIA MSIMAMO NDOA MIAKA 14

by Shabani Rapwi
Mar 27, 2023
MOURINHO KOCHA BORA WA KARNE – ÖZIL
HABARI

MOURINHO KOCHA BORA WA KARNE – ÖZIL

by Shabani Rapwi
Mar 27, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
August 2022
M T W T F S S
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031  
« Jul   Sep »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In