Wilaya ya Jimei huko Xiamen ilitangaza majaribio hayo mwishoni mwa julai kwa sababu ya hofu kwamba biashara haramu na wavuvi wa kigeni inaweza kuingiza virusi kutoka nje, kulingana na ripoti za ndani utaratibu huo unahusisha kupima watu na vitu ambavyo wamekuwa wakishulika navyo, ikiwa ni pamoja na samaki waliovuliwa majini.
Matokeo yake ni kwamba katikati, video zimeonekana kwenye mitandao ya kijamii inayoonyesha samaki wakipimwa vipimo vya UVIKO-19, inaweza kuonekana kuwa isiyo ya kawaida lakini hii sio mara ya kwanza kwa samaki walio hai kupimwa UVIKO-19.

Mfanyikazi katika Ofisi ya Maendeleo ya Bahari ya Manispaa ya Xiamen aliliambia gazeti la South China Morning Post: “Tumejifunza kutoka sehemu ya Hainan, ambayo inashuhudia mlipuko mbaya UVIKO-19.
Zaidi ya watu milioni tano waagizwa kufanyiwa uchunguzi wa UVIKO-19 katika mji wa pwani wa China wa Xiamen wiki hii, baada ya kesi 40 za virusi hivyo kugunduliwa.