Timu ya Wanawake ya Simba (Simba Queens) imeibuka na ushindi wa 5-1 dhidi ya AS Kigali ya Rwanda katika mchezo wa nusu fainali ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika ukanda wa CECAFA uliopigwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
–
Mabao ya Simba Queens katika mchezo huo yamefungwa na Aquino Corazone aliyefunga mabao mawili, Opa Clement, Aisha Juma pamoja na Diana William.
–
Simba Queens imetinga fainali na itachuana na She Corporate ya Uganda iliyotinga hatua hiyo kufuatia ushindi 2-1 dhidi ya Commercial Bank. Mchezo wa Fainali na wa kutafuta mshindi wa tatu zote zitapigwa Agosti 27, 2022 katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi.