
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson ameguswa na kupongeza jitihada za Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) katika kuboresha sekta ya kilimo hapa nchini kupitia huduma mbalimbali zinazotolewa na Benki ya NBC kwa wadau wa sekta ya kilimo.
Akizungumza wakati alipotembelea banda la Benki ya NBC kwenye Maonesho ya Kilimo Nanenane yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya, Dkt Tulia alionyesha kuvutiwa zaidi na huduma ya Bima ya Kilimo inayotolewa na Benki ya NBC kwa kushirikiana na kampuni ya Bima ya Jubilee ikilenga kuwalinda wakulima, wavuvi na wafugaji nchini dhidi ya hasara pindi wanapopata majanga mbalimbali yanayoweza kuathiri uzalishaji wao.