Tanzania imejihakikishia medali ya pili kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola msimu huu baada ya bondia, Yusuf Changalawe kushinda jioni ya jana Jumatano.
–
Changalawe amemchapa kwa Knock Out Arthur Langlier wa St Lucia na kutinga nusu fainali kwenye uzani wa juu mwepesi
–
Hata kama atapigwa kwenye hatua hiyo, Mtanzania huyo amejihakikishia medali kwa mujibu na kanuni za ngumi za ridhaa.
–
Kanuni hizo zinawatambua mabondia waliopigwa kwenye nusu fainali kuwa washindi watatu huku wale walioshindwa kutinga fainali ili kupata bingwa na mshindi wa pili.
–
Changalawe anakuwa Mtanzania wa pili kushinda medali kwenye mashindano hayo baada ya ile ya marathoni ya fedha hivi karibuni alipomaliza wa pili mbio ndefu za barabarani.