
Tottenham huenda ikamgeukia winga wa Wolves Adama Traore, 26, ikiwa hawataweza kufikia makubaliano na Roma kwa ajili ya kumnunua kiungo wa kati wa Italia Nicolo Zaniolo, 23. (90min)
Kiungo wa kati wa England Phil Foden, 22, amekubali mkataba mpya wa muda mrefu wenye thamani ya pauni 225,000 kwa wiki katika klabu ya Manchester City.. (Mail)
Manchester United na Chelsea wanamfuatilia mshambuliaji wa Leicester City Muingereza Jamie Vardy, 35, ambaye amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake wa sasa. (90min)
Dau la Brentford la pauni milioni 16.7 kumnunua kiungo wa kati wa Denmark Mikkel Damsgaard, 22, limekubaliwa na Sampdoria. (Sky Sports)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Mchezaji wa Man United Cristano Ronaldo
Klabu moja ya Saudia imesema kwamba ofa yao ya kumnunua mshambuliaji wa Manchester United na Ureno Cristiano Ronaldo, 37, itasalia mezani baada ya Kombe la Dunia iwapo mustakabali wa mchezaji huyo hautasuluhishwa.. (CBS Sports)
Manchester City wameanza mazungumzo na Anderlecht kuhusu beki wa kushoto wa Uhispania mwenye umri wa chini ya miaka 21 Sergio Gomez, 21, kama mbadala wa mchezaji waa Brighton, Mhispania Marc Cucurella, 24. (Times – subscription required)
Brighton wanamfikiria beki wa pembeni wa RB Leipzig Mhispania Angelino kuchukua nafasi ya Cucurella, ambaye pia amewavutia Chelsea. (Sky Sports Germany, via Mail)
Leicester wamekataa ofa ya pili, yenye thamani ya zaidi ya pauni milioni 40, kutoka kwa Newcastle kwa ajili ya kiungo wa kati wa Uingereza James Maddison, 25.. (Sky Sports)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,James Madisson
Kikosi hicho cha Eddie Howe pia kinamlenga winga wa Leicester na Uingereza Harvey Barnes, 24. (Guardian)
Beki wa Leicester Wesley Fofana amedokeza kuhusu hatua yake ya kuondoka uwanja wa King Power Stadium kwa kuiondoa akaunti ya Leicester City kwenye mtandao wake wa kijamii. Chelsea wameonyesha nia ya kumnunua Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 21 msimu huu wa joto. (Leicester Mercury)
Fulham wamewasilisha ofa ya kumnunua mlinzi wa Manchester United na Ivory Coast Eric Bailly, 28. (Football Insider)
Chelsea wana nia ya kumsajili beki wa pembeni wa Southampton na England Kyle Walker-Peters, 25. (Guardian)
Everton hawana nia ya kumsajili tena kiungo wa kati wa Uingereza Ross Barkley, 28, au mshambuliaji wa Ubelgiji Michy Batshuayi, 28, licha ya kuhusishwa na wachezaji hao wa Chelsea. (iSport)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Sevilla wanakaribia kumnunua beki wa kushoto wa Manchester United na Brazil Alex Telles, 29. (Fabrizio Romano)
Mlinzi wa Chelsea Mfaransa Malang Sarr angependelea kuhamia Monaco kuliko Fulham, ambayo inamlenga mchezaji huyo wa miaka 23. (Standard)
Sheffield United wako katika mstari wa mbele dhidi ya Brighton, Southampton na Leicester ili kumsajili kiungo wa kati wa Manchester City na England mwenye chini ya umri wa miaka 21 James McAtee, 19. (Athletic – subscription required)
SOURCE: BBC SWAHILI